
Kabla ya kusomwa kwa maelezo ya kesi hiyo ambapo Lulu hakutakiwa kujibu chochote kutokana na Mahakama ya Kisutu kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, Hakimu wa Mahakama ya Kisutu Augustina Mmbando amemtaka wakili wa serikali kutaja idadi ya mashahidi watakaotoa ushahidi wao wakati kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa.
Wakisoma kwa awamu maelezo ya mashahidi wa kesi hiyo, mawakili wa serikali kwenye hiyo kesi wamesema wanao mashahidi tisa wanaotarajiwa kuwatumia kwenye kesi na kuongeza kwamba shahidi namba moja ni Seth Bosco mdogo wa Marehemu Kanumba waliekua wakiishi pamoja.
Kwenye maelezo yaliyosomwa na Seth mahakamani, imeelezwa kwamba siku ya...