Pages

Mahakama Yaruhusu Mau Mau Kuishtaki Uingereza


DarSlam
Baadhi ya wazee wa Mau Mau
MAHAKAMA nchini Uingereza imetoa maamuzi kuwa wazee watatu wa Kenya ambao waliteswa na majeshi ya utawala wa kikoloni wa Uingereza wanaweza kufungua mashtaka dhidi ya Serikali ya Uingereza, na hivyo kuendelea mbele madai yao mengine ya ukatili. Maamuzi hayo yametolewa Oktoba 05, 2012 katika mahakama hiyo mjini London.
Serikali ya Uingereza ambayo kwa miaka mitatu imekuwa ikiajribu kuzuia hatua zozote za kisheria kuchukuliwa, imesema leo kuwa imesikitishwa na uamuzi huo na kwamba inapanga kukata rufaa. Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza imesema kuwa haipingi kuwa kila mdai wa kesi hiyo alinyanyaswa na kuteswa wakati wa utawala wa kikoloni, lakini hata hivyo itakata rufaa kutokana na kwamba maamuzi hayo yanaweza kuwa na madhara makubwa ya kisheria.
Wazee hao Paulo Nzili mwenye umri wa miaka 85, Wambugu Wa Nyingi mwenye umri wa miaka 84 na Jane Muthoni Mara mwenye umri wa miaka 73, walifanyiwa ukatili wa

Rais Jakaya Mrisho Kikwete Apokea Jezi Toka kwa Waziri Mkuu wa Canada

DarSlam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi toka kwa Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo, Alhamisi Oktoba 4, 2012