Ujio wake kwenye gemu
uliambatana na msisimuko. Ngoma za masikio ya vichwa vya Hip Hop Bongo
zikaanza kuwambwa upya kujiandaa kupokea mitetemeko inayotoka kwenye koo
la One. One The Incredible.
Wakati ana miaka kama sita hivi, kaka zake walikuwa wanakutana na wasanii kama kina SOS B,
na wakongwe wengine kwenye gemu la Hip Hop Tanzania miaka ya 90, kupiga
tizi na kubadilishana ujuzi. Sidhani walikuwa wanatambua kuwa
wanatengeneza Muujiza utakaokuja kushangaza watu miaka 20 baadae. Na
muhimu zaidi, kusimamia nguzo zilizosimamishwa na waliotangualia.
Leo hii One anajitambua na anatambulika kama Kijana mwenye Kipaji na Mzawa wa Tanzania.
One anategemea kufyatua mzigo wa nyimbo 24 wiki ijayo utakaokwenda
kwa jina la “Soga Za Mzawa”. Bahati nzuri, tulipata muda wa kulonga naye
na kujenga mambo mawili matatu…
1. Niambie Moko wa Miujiza?
Shwari.
2. Kwanza kabisa, kwanini uliamua kujiita “One” au “One The Incredible” au “Moko wa Miujiza”? Jina ulilipata wapi?
One ni jina nililopewa na mentor wangu at the time, Lord’s Child aka L.C. Yeye aliamua kuniita hivyo kutokana na flow na uandishi wangu.
3. Kitu gani kilikusukuma kuingia kwenye gemu, au watu gani walikusukuma mpaka ukashtukia unaliweza gemu?
Kikubwa hasa kilikuwa ni kaka zangu… R.I.P. Wao ndio walinitambulisha kwa rap. Baadae ikaja kuwa interest
yangu baada ya kugundua hicho ndicho kitu pekee ambacho kila mtu
alikuwa akinipongeza kwa uwezo niliokuwa nao, vitu nilivyokuwa nafanya.
Basi nikaamua..