Padre wa Kanisa Katoliki Zanzibar Anselmo Mwan'gamba Amwagiwa Tindikali (Video)
Kwa mara nyingine Zanzibar imeshuhudia tukio la kumwagiwa tindikali ambapo watu wasiojulikana wamemwagia tindikali Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mpendae,Padri Anselmo Mwan'gamba na kumjeruhi sehemu ya uso na mwilini.
Behind the Rhymes of Khaligraph Jones #theTrend
Larry Madowo spoke to Brian Robert Ouko otherwise known as Khaligraph Jones, the HipHopper about his life and music.
Ottomatic and Khaligraph Jones - Beat goes on (Feat. Shamir)
KAMATA FURSA TWENDZETU KWA VIJANA SEMINA ILIYOFANYIKA DODOMA

Msanii mahiri wa Kughani Mashairi kwa mtindo wa kisasa kabisa,Mrisho mpoto akizungumza mbele ya sehemu ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma na vitongoji vyake waliojitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya kamata Fursa twendzetu,iliofanyika ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma. Semina ya Kamata Fursa twendzetu inayoratibiwa na Clouds Media Group,imekwishafanyika mikoa zaidi ya mitano ikiwemo Kigoma,Tabora,Singida,Mtwara,Mbeya,Iringa sambamba na leo ndani ya Dodoma,ambo semina hizo zote zimeonesha mafanikio makubwa kwa vijana kwali walikuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye ushiriki.

Sehemu ya washiriki wa semina hiyo ilipokuwa ikiendelea mapema leo asubuhi.


Wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye semina hiyo ya kamata fursa twendzetu,mapema leo asubuhi mkoani Dodoma.

Mwakilishi wa NSSF-Makao Makuu,Salim Khalfan akifafanua masuala mbalimbali yatokanayo na faida za kujiunga na shirika hilo la NSS,ndani ya semina ya kamata fursa twendzetu iliofanyika mapema leo kwenye moja ya ukumbi wa hotel ya Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi


Sehemu ya ya watu wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri kwenye semina hiyo.

Meneja wa NSSF mkoani Dodoma,Bwa.Kirondera Nyabuyenze akizungumza fursa mbalimbali zitokanazo na shirika la NSSF,Nyabuyenze amewataka watu mbalimbali wajitokeze kwa wingi kujiunga na NSSF,ili kujipatia fursa mbalimbali zikiwemo mikopo,matibabu na mambo mengiyo mbalimbali.

Mwakilishi wa Kampuni ya Maxmalipo,Renard Munuri akizungumza kwenye semina ya Kamata Fursa Twenzetu kwa vijana,kuhusiana na masuala mbalimbali yanayofanywa na kampuni yake katika kusaidia huduma za jamii,ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Mmoja wa Watangazaji mahiri wa Clouds FM,akizungumzia fursa mbalimbali alizokumbana nazo na namna alivyozifanyia kati na kujipatia sehemu ya mafanikio katika kupambana na maisha.Semina ya Kamata Fursa twendzetu inayoratibiwa na Clouds Media Group,imekwishafanyika mikoa zaidi ya mitano ikiwemo Kigoma,Tabora,Singida,Mtwara,Mbeya,Iringa sambamba na leo ndani ya Dodoma,ambo semina hizo zote zimeonesha mafanikio makubwa kwa vijana kwali walikuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye ushiriki.

Baadhi ya wasanii ambao wamenufaika mara baada ya kujiunga na Shirika la NSSF,shoto ni Queen Doreen na Mwasiti wakijadiliana jambo na mdau Phillipon mapema leo,wakati semina ya Kamata fursa twendzetu ilipokuwa ikiendelea.

Sehemu ya wakazi wa mji wa Dodoma wakiwa wamejitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya fursa kwa vijana

Sehemu ya meza kuu ya watoaji mada wakishangilia jambo.
Woman Uses Fake Baby Bump in Attempt to Smuggle Cocaine
Pictured: The fake baby bump used by a Canadian woman social worker 28, caught smuggling two kilos of cocaine out of Colombia
Tabitha Leah Ritchie was carrying over four pounds of cocaine under a latex belly
Colombian police detained her after an inspector noticed her belly was cold and hard
Ritchie is a social worker who arrived in Colombia on August 6.
Tabitha Leah Ritchie was carrying over four pounds of cocaine under a latex belly
Colombian police detained her after an inspector noticed her belly was cold and hard
Ritchie is a social worker who arrived in Colombia on August 6.
Ni Kweli Watu Hawana Uwezo wa Kunisaidia Ili Nisife
Inauma sana unapoona familia ndio inakutegemea, halafu unayetegemewa mwenyewe unaumwa kama hivi.Mbaya zaidi kadri ninavyohangaika ili kupona, hali ndio inazidi kuwa mbaya zaidi. Nimekuwa nikitokwa na usaa mwingi mno, kwa dakika tu hata kikombe kinajaa, nilikwenda hospitali wamezuia hilo.Sasa uvimbe naona unakua, maumivu ninayoyapata ni makali mno.Naombeani mniokoe nipate fedha nikatibiwe.
Joseph Ayubu ni mkazi wa Kijiji cha Nyenze, Shinyanga.Ugonjwa unaomsumbua unaendelea kumwathiri, huku akiwa hana uwezo wa matibabu.
Maisha yamejaa changamoto, unaweza kulia kwa sababu ya tatizo hili, mwingine akalia kwa lile.
Wataalamu wa saikolojia, wakiwemo Fernald LD na Hockenbury Hockenbury kutoka New Zealand, wanasisitiza katika machapisho yao kadhaa yakiwemo kitabu cha Life is like this, yaani maisha ni kama hivi, kwamba unapokuwa na tatizo, tuliza kichwa, tafakari sababu hasa ni nini na nini cha kufanya ili kuondokana na hali hiyo.
Ilimradi uko hai, shida zipo, huna sababu ya kukata tamaa, cha msingi chukua hatua kuzishinda shida zinazokusumbua, ikiwezekana shirikisha wengine.
Mfano wa Joseph Ayubu
Joseph Ayubu (40) mkazi wa Kijiji cha Nyenze wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga, kwa miaka mingi amekuwa akihangaika kupata tiba ya tatizo lake bila mafanikio.
Ayubu anateswa na ugonjwa wa kansa, hali yake kwa sasa ni mbaya, anatokwa na usaa mwingi; akiukinga usaha unaotoka shingoni, kikombe hujaa ndani ya dakika moja.
“Nimevumilia mno, kadri siku zinavyokwenda mbele naona kifo kinakuja. Sitaki kuamini kama ulimwengu wote au Watanzania wote wanaweza kuwa na roho ngumu ya kushindwa kuniokoa, naomba msaada niondokane na shida hii,” anasema Ayubu.
Anawaomba wasamaria wema wamchangie fedha ili akatibiwe katika Hospitali ya KCMC iliyoko mkoani Kilimanjaro.
Ayubu anasumbuliwa na tatizo la saratani ya shingo, hivyo kusababisha shingo yake kuvimba na kumfanya ashindwe kutoa sauti ipasavyo kwani sehemu kubwa ya koo lake imeziba.
Anaeleza kuwa kutokana na ugonjwa huo, kichwa nacho kinazidi kuvimba na kupata maumivu makali.
Macho nayo yanavimba na kumsababishia ashindwe kuona mbali. Mbaya zaidi ni kwamba kwa namna anavyoona, kila siku ugonjwa unaendelea kukua katika mwili wake.
Anasema ugonjwa huo umeshindikana kutibiwa katika hospitali za kawaida hivyo anatakiwa aende kutibiwa Hospitali ya KCMC (Kilimanjaro Christian Medical Centre).
Ayubu anatakiwa kuchomwa sindano sita, kila sindano gharama yake Sh218,000, hivyo anatakiwa awe na Sh1,308,000 kwa matibabu hayo pekee, nje ya tiba zingine, gharama za kuishi huko KCMC na mengineyo.
Ugonjwa ulivyoanza
Alianza kuugua maradhi hayo mwaka 2010, ulianza uvimbe mdogo shingoni, baadaye ukaongezeka, ikamlazimu kununua dawa za kutuliza maumivu hasa Panadol, kwa vile uvimbe huo ulikuwa unasababisha maumivu makali.
“Hali yangu ya kiafya inazidi kudhoofika, siwezi tena kufanya kazi za kuniingizia kipato kwani maumivu ninayoyahisi ni Mungu tu ndio anajua, ni maumivu makali mno. Ninaomba sana Watanzania wenzangu na yeyote ambaye si Mtanzania anisaidie, nina mke na watoto ambao bado wadogo na sina namna ya kuwasaidia kwa sasa”anasema.
“Wakati mwingine mwili wangu unakufa ganzi na fahamu kupotea, wakati mwingine fahamu zinarudi naweza kujielewa vizuri, ninachokisubiri kwa sasa ni huruma yenu Watanzania, ndiyo itasababisha maisha yangu kurudi kama nilivyokuwa mwanzo”
Anasema watoto wake wanasoma lakini kwa sasa wamesimamishwa kwa sababu hana fedha za kuwalipia ada na huduma zingine za masomo.
Anasema alipokuwa hajaugua ugonjwa huo alikuwa akifanya shughuli mbalimbali ndogo ndogo za kuingiza kipato, huku akifanya pia kazi kama Mwalimu wa Kwaya katika Kanisa la KKKT kijijini hapo. Kwa sasa hawezi tena kufanya kazi yoyote kwa sababu ya maumivu makali anayohisi na pia hali ngumu ya kiafya inayoendelea kumsumbua.
“Nimeshawahi kwenda hospitali mbalimbali mkoani hapa lakini hali haibadiliki, nilienda hadi kwa waganga wa kienyeji, ugonjwa unaongezeka.
Hali yake kwa sasa ni mbaya, ndani ya dakika moja naweza kujaza usaha kwenye kikombe, huku maumivu yakiendelea kuwa makali zaidi.
Ayubu anasema ameendelea hivyo, mpaka alipokwenda Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga, ambako alishonwa ndipo angalau sasa usaha umepungua, ingawa hali yake bado ni mbaya hasa shingo kuendelea kuvimba.
“Mpaka sasa siwezi kugeuka nikitaka kugeuka inabidi nigeuze mwili wote sio siri nateseka sana endapo maumivu haya yangekuwa yanawezekana kumwachia mtu mwingine ningekupa ukaona maumivu yake.
“Nina watoto wananitegemea, nilikuwa nalima na kufanya biashara mbalimbali, kwa sasa siwezi kutokana na kupata maumivu makali ambayo yananisababishia hata kushindwa kula”anasema Ayubu.
Maisha yake kwa sasa yamekuwa ya kubahatisha, kuna wakati hulala bila kula japo ni mgonjwa.
“Sisi Watanzania wote ni ndugu nihurumieni mwenzenu naumia, naomba sana mnisaidie kulingana na ulichonacho,”anasema Ayubu huku akitokwa machozi.
Kwa mujibu wa Ayubu, madaktari wamemshauri kwamba akipata fedha hizo tatizo lake linaweza kutibiwa na kurudi katika hali yake ya kawaida.
Kwa mujibu wa vitabu vitakatifu, kusaidia wenye uhitaji huchangia kupata baraka katika maisha, lakini kama wanadamu tunapaswa kusaidiana...duniani tunapita.
Kwa yeyote mwenye moyo wa kumsaidia chochote, Ayubu awasiliane na Mhariri wa Jarida la Ndani ya Habari, 0754498972.
Mwananchi
Alex Massawe Huenda Akapanda Kizimbani Dubai
Massawe anayetarajiwa kuletwa nchini wakati wowote kuanzia sasa, alikuwa anatafutwa na Polisi wa Tanzania kwa muda mrefu na alikamatwa Dubai, mapema Julai na maofisa wa usalama wa UAE baada ya alama zake za vidole kuonyesha kuwa alikuwamo kwenye orodha ya watu waliokuwa wanasakwa na Interpol.
Baada ya kukamatwa, Mkuu wa Interpol, Tawi la Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Gustav Babile alisema Massawe alikamatwa kati ya Juni 20 na 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai akitokea Afrika Kusini.
Massawe ambaye anafanya biashara zake katika Miji ya Arusha, Dar es Salaam na Moshi, inadaiwa kwamba akiwa Dubai, alikutwa na pasi tatu bandia za kusafiria zilizokuwa na majina tofauti wakati alama zake za vidole zilionyesha anaitwa Alex Massawe. “Ombi la kuleta mhalifu nchini kutoka nje ya nchi (extradition request), lina hatua ndefu. Unajua kuna mlolongo wa taratibu za kutekeleza. Kwanza lazima Polisi wa Tanzania watoe tangazo kwa Interpol kuhusu kumsaka mtu huyo ili aletwe,” alisema Babile.
Hivi karibuni, Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu Dar es Salaam ilitoa hati ya kukamatwa na kurejeshwa nchini kwa Massawe ili kukabiliana na kesi mbili ikiwamo ya madai ya kughushi nyaraka mbalimbali.Kusoma zaidi bofya
Hati hiyo ilitolewa baada ya Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka kuwasilisha ombi la kutaka mfanyabiashara huyo arejeshwe nchini kwa kuwa tayari amefunguliwa kesi namba 150/2013.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna wa Polisi, Robert Manumba alisema kwa agizo hilo, polisi kupitia kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliandika barua kwa Mwanasheria Mkuu wa Dubai kuangalia taratibu za kisheria za kumrudisha baada ya kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo.
“Massawe alifikishwa mahakamani Dubai kwa makosa ya kukutwa na hati bandia za kusafiria, lakini vilevile kugundulika kuwa ni kati ya watu wanaotafutwa na Polisi wa Interpol kwa tuhuma za mauaji,” alisema Manumba.
“Sheria inasema mtu akikamatwa nchi nyingine, anashtakiwa nchini humo, huku taratibu za kisheria za kumrejesha zikiendelea kwa nchi ambazo zina utaratibu wa kubadilishana wafungwa kama ilivyo Tanzania na UAE,” alisema Manumba.
Alisema ushahidi dhidi ya mtuhumiwa huyo umekamilika na tayari umewasilishwa Dubai ili kuendelea na taratibu nyingine za kisheria za kumrejesha Tanzania haraka kujibu tuhuma zinazomkabili.
Kutajwa mahakamani
Aprili 4, mwaka huu, Massawe alitajwa mahakamani katika kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Onesphory Kituly ambaye aliuawa katika mazingira ya kutatanisha Novemba 6, 2011 akiwa nyumbani kwake Magomeni, Dar es Salaam.
Katika kesi hiyo ambayo mshtakiwa wa kwanza ni mfanyabiashara maarufu, Abubakar Marijani ‘Papaa Msofe’, mshtakiwa mwingine, Makongoro Joseph Nyerere alitoa malalamiko, mbele ya Hakimu Mkazi, Agnes Mchome mara baada ya Wakili wa Serikali, Mwanaisha Kombo kudai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe mpya ya kuitaja.
Mshtakiwa huyo, aliomba jalada la kesi yao lipelekwe mahakamani hapo kwa ajili ya kulifanyia kazi na kutuhumu kuwa ndugu wa marehemu Kituly hawataki maendeleo ya kesi yao hadi Massawe akamatwe.
Mwananchi
Subscribe to:
Posts (Atom)

