Pages

Bongo Blogs: Blog Zote za Tanzania Sasa Zinapatikana Ndani ya Blog Moja (Directory)

Tanzania Directory 
Acha kuzunguka blog kibao bila kupata habari uliyokua unaitafuta,  Blog ni moja tu Bongo Blogs ndio unatakiwa kukumbuka halafu nyinginezo zooote utazipata ndani yake (Bongo Blogs) bofya link..
 >> Bongo Blogs
 http://bongoblogs.blogspot.com
Blog yako ya Taifa

Banana Zoro -Jirani (Audio)

Banana Zoro-Jirani

Expert Valves: ..The India Show in Tanzania -Invitation

Expert Valves

RASHID MATUMLA AFUNGUKA KUHUSU TUHUMA ZINAZOMKABILI MDOGO WAKE

RASHID MATUMLA Bondia Rashid ‘Snake man’ Matumla amedai endapo itathibitika mdogo wake, Mkwanda anajihusisha kusafirisha dawa za kulevya atakuwa ameipa fedheha familia yao.

“Mkwanda ameipa fedhea familia yetu, hii ni aibu kubwa ukizingatia vitendo hivyo vinakatazwa si Tanzania tu bali na kwenye nchi nyingine,” alisema Matumla jana katika mahojiano na gazeti hili.

Mkwanda ambaye kwa mujibu wa Rashid alipumzika kucheza ngumi miaka kadhaa iliyopita kutokana na kusumbuliwa na maradhi alikamatwa wiki iliyopita nchini Ethiopia akiwa na mchezaji wa zamani wa Simba, Joseph Kaniki na leo watapandishwa kizimbani nchini humo kwa tuhuma hiyo.

“Mimi mwenyewe nashangaa ni lini amejiingiza kwenye kazi hiyo, hata wakati anaondoka hakuniaga, mimi kaka yao na familia hatuelewi chochote,” alisema Matumla.

Alisema mdogo wake huyo alikuwa amebadilisha uraia na kuchukua uraia wa Sweden na kuoa hukohuko Sweden licha ya kwamba hapa Tanzania alikuwa amepanga Mbagala, Dar es Salaam na alikuwa anakuja na kukaa kwa muda na kisha kuondoka.

“Ni mwezi sasa umepita sina taarifa naye na hata wakati anaondoka hakuniaga, nimesikia kupitia vyombo vya habari kitendo cha mdogo wangu kukamatwa kimenisikitisha mno, siyo siri nimekwazika na ninarudia kusema hii ni fedheha kwenye familia yetu,” alisema bingwa huyo wa zamani wa dunia wa WBU. Rekodi zinaonyesha kabla ya kupumzika kwa muda kucheza ngumi, Mkwanda alishinda mapambano manane (sita kwa KO) alipigwa mara tatu zote kwa KO alitoka sare mara moja tangu 2004.
MWANANCHI

Mnyarwanda AJINYONGA Baada ya Kuamriwa Arudi Kwao RWANDA..!

RWANDA
Raia wa Rwanda amejinyonga kwa kamba chumbani kwake, tukio linalohusishwa na zoezi linaloendelea hivi sasa nchini la kuwasaka wahamiaji haramu na kuwarejesha makwao.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio, marehemu anatajwa kuwa ni Francis Mathias (75), ambaye alikuwa mkazi wa kitongoji Kikukuru kata Kikukuru, tarafa Mabira wilayani Kyerwa mkoani Kagera.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Kikukuru, Joseph Leo, jana alilithibitishia NIPASHE kutokea kwa tukio hilo na kuwa alipata taarifa hizo kutoka kwa binti wa marehemu juzi saa 3:00 asubuhi.

“Baada ya kupata hizo taarifa niliongozana na mgambo, tulipofika mlango wa chumba chake ulikuwa umefungwa kwa ndani, tukafanikiwa kuuvunja tukaingia ndani na kukuta amejitundika kwa kamba,” alisema Leo na kuongeza kuwa marehemu alikuwa mfugaji na mkulima.
Alisema kuwa kabla ya kujiua, mzee huyo alichana fedha za Kitanzania zinazokadiriwa kufikia Shilingi
milioni saba zikiwamo noti za Sh. 5,000 na za Sh. 10,000, ambazo zilikutwa ndani ya chumba chake.

Leo alisema baada kushuhudia alipiga simu kwa Ofisa Mtendaji wa Kata Kikukuru ambaye alifika na kupiga ngoma na watu walikusanyika kushuhudia kilichotokea na baadaye kwenda kutoa taarifa katika kituo cha Polisi.

Alipotakiwa na NIPASHE kuthibitisha kama kweli mwananchi wake aliyejinyonga alikuwa raia wa Rwanda, Leo alithibitisha na kufafanua kuwa tayari alikwisha kumuorodhesha kwa lengo la kurejeshwa kwao katika opereshani iliyoanza Jumamosi ya kuwarejesha makwao wahamiaji haramu wanaoishi mkoani Kagera.

Aliongeza kuwa aliwahi kumhoji marehemu Mathias ambaye alimweleza kuwa alikuja Tanzania kutoka Rwanda tangu mwaka mwaka 1976.

Naye Ofisa Tarafa ya Mabira, Nicolaus Rugemalira, alisema uchunguzi wa awali wa kimazingira umeonyesha kuwa kulikuwa na mgogoro wa familia baada ya marehemu kutaka wauze mali zao zote warudi Rwanda, lakini familia yake haikukubaliana naye kutokana na mkewe kuwa raia wa Tanzania.

“Mke wake ni Mtanzania, inaonekana baada ya familia yake kukataa uamuzi wake wa kuuza mali zote ili waondoke, aliamua kuchukua uamuzi huo,” alisema Rugemalira.

Akizungumzia tukio hilo, binti wa marehemu, Melania Francis, alithibitisha kuwapo ugomvi kati ya baba yake na mama yake hali iliyosababisha mama yao kuondoka bila kufahamika alikoelekea.

Alisema siku ya tukio aliamka na kuwaandaa wadogo zake kwenda shuleni na baada ya hapo alikwenda shambani kuona kama vibarua wameanza kazi ya kulima, lakini aliporudi nyumbani alishangaa kuona mlango wa chumba cha baba yake bado umefungwa wakati haikuwa kawaida yake kulala hadi saa moja.

Melania alisema alibisha hodi bila majibu, akajaribu kufungua ikashindikana na alipochungulia aliona fedha nyingi zimetapakaa ndipo alipokimbia kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa kitongoji.

“Nafahamu baba alikuwa na uwezo wa kumiliki fedha hizo, lakini sikufahamu anazihifadhi wapi,” alisema binti huyo wa marehemu.

Alisema wamezaliwa watoto watano katika familia hiyo na kwamba ndugu zake wawili walitoweka na kubakia watatu na kuongeza kuwa kuwa anatambua kuwa baba yake alikuwa raia wa Rwanda.

Alipotakiwa kueleza kama anafahamu alikoelekea mama yake, binti huyo alidai kuwa hafahamu ingawa anafahamu kuwa ni mzaliwa wa Wilaya ya Ngara, mkoani Kagera.

Kutokana na kutoweka kwa mama huyo pamoja na wanafamilia wengine, uongozi wa eneo hilo unaendelea na ufuatiliaji ili kujua wanafamilia wengine wamekwenda wapi. 
NIPASHE

KATUNI ya Juzi

BAADA ya KUPIGWA STOP, FID Q ALIRUDISHA DARASA la HIPHOP kwa KASI ya AJABU

Farid Kubanda aka Fid Q aka Ngosha The Don 
Farid Kubanda aka Fid Q aka Ngosha The Don, he’s a real Hip Hop super star hapa Bongo baada ya mangoma yake kibao ku-bang kwa hewa.

Fid Q decided kuanzisha darasa la Hip Hop kwa lengo la kuwapa skillz wasanii katika utungaji pamoja na kufokafoka.
Lakini wakati Kubanda akiwa kwenye mission yake mwenye nyumba aliamua kumpiga bonge la boot na kumwonyesha mlango wa kutokea fastafasta.
Kweli baada ya Ngosha kustopishwa class pia ilisimama, lakini Fid Q sio mtu wa ku-give up coz currently ameongea na BK Cop kuhusu hilo:

“Narudisha darasa langu la hip hop baada ya sehemu niliyokodi mwazo kuwa na magumashi ya kupandishiwa kodi na nikaona ni-stop ku-provide ma-skillz, but now nimepata place maeneo ya TMJ Mikocheni na pako very suitable kwa wanafunzi.” Ngosha ze swagger Don added to BK Cop, “Class itaanza soon na wanafunzi 35 wapo permanently so ninawakaribisha na wengine wote who likes Hip Hop”

Bob Marley - Coming In From The Cold with Lyrics ..The Legend.

Lyrics:
In this life, in this life, in this life,
In this, oh sweet life:
We're (we're coming in from the cold);
We're coming in (coming in), coming in (coming in),
coming in (coming in), coming in (coming in),
Coming in from the cold.

It's you - it's you - it's you I'm talkin' to -
Well, you (it's you) - you (it's you) - you I'm talking to now.
Why do you look so sad and forsaken?
When one door is closed, don't you know other is open?

Would you let the system make you kill your brotherman?
No, no, no, no, no, no! No, Dread, no!
Would you make the system make you kill your brotherman?
(No, Dread, no!)
Would you make the system get inside your head again?
(No, Dread, no!)
Well, the biggest man you ever did see was - was just a baby.

In this life (in this life),
In this (in this life, oh sweet life):
Coming in from the cold;
We're coming in (coming in), coming in-a (coming in),
coming in (coming in), ooh! (coming in)
Coming in from the cold!

It's life (it's life), it's life (it's life), it's life (it's life):
it's - wa - well! - coming in from the cold!
We're coming in (coming in), coming in (coming in) -
ooh (coming in), hey! (coming in),
Coming in from the cold!

It's you - you - you I'm talking -
Well, yes, you, bilyabong! (it's you);
ew! - you I'm talking to now.
Gi-irl, why do you look so - look so - look so sad -
look so sad and forsaken?
Don't you know: When one door is closed - when one door is closed,
many more is open?

We-e-e-ell, would you let the system get inside your head again?
No, no, no, no, no, no, no, no, no, Dread, no!
Would you let the system make you kill your brotherman?
No, Dread, no!
We-e-e-ell, would you make the system get inside your head again?
(No, Dread, no!) No, no, no, no, no, no, no, no, no, no!
Well, the biggest - biggest man you ever - ever
Did-a see was-a - was-a once a baby.

In this life, in this life, in this life,
In this, oh, sweet life,
We're (coming in from the cold) from the cold!
We're coming in (coming in), coming in (coming in),
coming in (coming in), wo-o! Yea-ea-eah!
Coming in from the cold

We're coming in-a, coming in-a, coming in-a, coming in-a!
Yeah, yeah, yeah, yeah, yea-ea-ea-eah!
Coming in from the cold
Coming in (coming in), coming in (coming in) -
(coming in) (coming in)
(coming in) from the - from the cold!
BONUS..

Bob Marley - Redemption Song

YG ft. Jeezy, Rich Homie Quan - My Nigga (Explicit)

Mirihini Witchcraft -Ukistaajabu ya Musa....