Pages

Young D -KIJUKUU (Audio)

Young D

Wake wa Viongozi wa Uamsho Wafunguka.

Viongozi wa Uamsho
Wake wa viongozi Jumuiya ya Uamsho Zanzibar, wameiomba serikali kuitazama kesi inayowakabili viongozi hao kwa jicho la uadilifu, haki na sheria ili kuonesha dhana ya utawala bora.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la wanawake wa Kiislamu lililofanyika msikiti wa Mbuyuni, kinamama hao wamelalamikia kesi hiyo kuchukua muda mrefu huku ikiwa hakuna hatua yoyote muhimu inayochukuliwa ili haki itendeke.

Wametaka vyombo vya sheria vifanye kazi kwa maadili, hasa ikizingatiwa kwamba Zanzibar ni mshiriki wa Muungano wa Tanzania ambayo ni mwanachama wa taasisi mbalimbali za kulinda na kuheshimu haki za binadamu ulimwenguni.

“Hatukusudii kuingilia kazi za mahakama, bali tunaeleza hali halisi ya uvunjwaji wa sheria na katiba ya nchi kwa vyombo vya sheria kufanya kazi kwa utashi bila ya kuzingatia haki za wanachi mbele ya sheria”, walidai wanawake hao.

Walidai kuwa, kitendo cha kunyima haki kinaweza kuitia doa kubwa mahakama na serikali mbele ya macho ya kimataifa.

Aidha, walitaja sababu za kuwekwa ndani waume zao kuwa ni harakati zakuongoza umma wa Wazanzibar kudai haki yao ya msingi juu ya hatima ya Zanzibar kuwa nchi yenye uhuru wa kujiamulia mambo yake.

Wameeleza kusikitishwa kwao kwa kusema kuwekwa ndani kwa waangalizi hao wa familia zao, kumewaathiri sana kisaikolojia na kiuchumi.

Pia wamesema mwenendo mzima wa taaluma za Kiislamu ambazo viongozi hao walikuwa wakifundisha katika madarsa mbalimbali kwenye misikitini na vyuo, umeathiriwa na kushikiliwa kwa viongozi hao.

Kwa hivyo wamevitaka vyombo vya sheria kufanya haki katika maamuzi yao ili kudumisha amani na utulivu uliopo pasi na kutia dosari serikali ya umoja wa kitaifa iliyowalea Wazanzibari pamoja.

Kupitia kongamano hilo, wanawake hao wameviomba vyombo vya sheria, kuwaruhusu viongozi hao kuonana na wake na ndugu zao wakati wanapofikishwa mahakamani kwa kusikilizwa kesi yao.

Katika hatua nyengine, kinamama hao wameunda kamati ya kufuatilia na kuratibu mwenendo wa kesi pamoja na kuonana na watendaji wa haki za binadamu.

East Africa Chamber of Commerce Trade Conference, Invitation

 East Africa Chamber of Commerce Trade Conference

Country Wiz Ft G Nako - Watch Me Mastering (Audio)

Country Wiz Ft G Nako - Watch Me Mastering

Quote of the Day

Quote

Wauza `Unga` Waiteka D`Salaam Airport

Oliver TamboNidhahiri kwamba Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), sasa ni kitovu cha kusafirisha dawa za kulevya nje ya nchi.
Katika kipindi cha takribani wiki mbili tu, Watanzania wanne wamekamatwa ughaibuni wakiwa na shehena ya dawa hizo ambazo walisafirisha kutoa Tanzania kwenda nje kupitia uwanja huo bila ya kukamatwa.

Mara ya kwanza walikuwa ni wasichana wawili, Agnes Jerald (25) na Melisa Edward (24), ambao walikamatwa Afrika Kusini na kushtakiwa nchini humo.
Walikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo wakiwa na shehena ya kilo 150 ya dawa aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8. Wasichana hao walikamatwa Julai 5, mwaka huu baada ya kuwasili Johannesburg wakitokea Tanzania wakisafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) na walikamatwa na Maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya nchi hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, uliopo eneo la Kempton Park.

Ijumaa wiki hii, Watanzania wengine wawili, walikamatwa Hong Kong wakiwa na dawa za kulevya aina ya cocaine na heroine zenye thamani ya bilioni 7.6 akiwamo mmoja aliyekamatwa akitokea Dar es Salaam kupitia Dubai hadi Honh Kong.

Matukio haya yote yanatokea wakati wakuu wa Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere zinakopitishwa wakiwa hawana cha kusema juu ya uharamia huo unaotokea kwenye kitovu cha mawasiliano cha nchi.

Jana, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Viwanja vya Ndege Nchini, Deusdedit Kato, alisema jalada la upelelezi kuhusu tukio la kukamatwa kwa wasichana Afrika Kusini litapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) leo ingawa hakuwa tayari kutaja watuhumiwa ni nani hasa wanaoshirikiana na wafanyabiashara ya dawa hizo.

Kato alisema hawezi kutaja majina ya watu waliobainika kwa sababu kilichofanyika ni uchunguzi tu na kwamba DDP ndiye mwenye mamlaka ya kuamua juu ya uchunguzi huo.

“Siwezi kukuambia ni nini kimepatikana katika uchunguzi wala kutaja majina ya watu, kwa kuwa mimi ninapeleka nilichokichunguza kwa sababu naweza kukuambia lakini ikawa sio hivyo kwani huu ni uchunguzi tu,” alisema.

Aliongeza: “Naweza kupeleka jalada langu la uchunguzi kwa DDP lakini kutokana na utalaam wake akagundua kuna mapungufu, hapo tayari nitakuwa nimepotosha umma. Lakini pia akiona upelelezi unajitosheleza yeye ndiye anaweza kuamua kupeleka Mahakamani.”

Kuhusu taarifa za kukamatwa kwa Watanzania wengine na dawa za kulevya Julai 26, mwaka huu huko huko mjini Hong Kong, Kato alisema bado wanafanya jitahada za kupata kwa undani taarifa hizo.

“Na mimi nimesikia, lakini hatujapata taarifa zaidi ili kujua majina yao na kama kweli ni Watanzania. Inakuwa ngumu kupata taarifa kwa sababu aina ya mawasiliano wanayotumia hawa Polisi wa Kimataifa (Interpol ) ni tofauti na ya kwetu kwa hiyo tunategemea wao ndiyo watupe taarifa,” alisema Kato.

Naye Waziri wa Uchunguzi, Dk. Harrison Mwanyembe, ambaye amejipatia sifa za utendaji katika siku za hivi karibuni, kwa kuendesha timua timua katika taasisi zinazosimamiwa na wizara yake kwa tuhuma za uzembe, amekuwa kimya na pengine kukwepa kabisa kutia mguu katika sakata la dawa za kulevya JNIA.

Wiki iliyopita NIPASHE lilimtafuta Dk. Mwakyembe mwenye dhamana ya Viwanja vya Ndege nchini kujua ni hatua gani amechukua, lakini alijibu kwamba hana taarifa za kina kuhusu sakata hilo.

Uharamia huo wa dawa za kulevya umempa pia kigugumizi Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba, ambaye amekwepa kuzungumzia sakata hilo na kusema liko kwa Kamanda wa Polisi, Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzowa.

Kamanda Nzowa alipoulizwa alisema upelelezi bado unaendaelea kubaini mambo mbalimbali yaliyoko nyuma ya tukio hilo.

Alipoulizwa ikiwa Polisi wamebaini mmiliki pamoja na maofisa walioruhusu kupitishwa kwa dawa, Nzowa alisema uchunguzi unaangalia mambo mengi na ndiyo huo utakuja na taarifa kamili.

Taarifa kutoka Hong Kong za Ijumaa wiki iliyopita zinaeleza kwamba, maofisa ushuru wa Uwanja wa Ndege wa Hong Kong (HKIA), walimkamata kijana mmoja mwenye umri wa miaka 26 akitokea Tanzania na alikuwa na dawa za kulevya aina ya heroin kilo 1.6 zenye thamani ya Sh. bilioni 1.5, kwenye mzigo wake wa mkononi.

Taarifa zilieleza kwamba baadaye jioni siku hiyo hiyo, maofisa hao walimkamata Mtanzania mwingine mwenye miaka 45 ambaye alipelekwa hospitali na kutolewa gramu 240 za dawa za kulevya aina ya heroin.
Taarifa zaidi zilieleza kuwa Mtanzania mwingine mwenye miaka 28 alikamatwa akiwa na kilo 2.03 za cocaine.

Takwimu zinaonyesha kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na uharamia huo.

Katika kipindi hicho, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, na kuharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.
NIPASHE

Watch Mkasi with Mh A.Mwinyi

Vunjika Mbavu KinaiJeria Style

Biggie Boss ft. Cpwaa & Julio Big Brother - Amsha (Audio)

Biggie Boss, Cpwaa, Julio Big Brother, Amsha

RAIS PAUL KAGAME HATARINI KUSHITAKIWA ICC


ONYO lililotolewa na Ikulu ya Marekani dhidi ya Serikali ya Rwanda, linalomtaka Rais wa nchi hiyo, Paul Kagame, kuacha kuwasaidia waasi wa kikundi cha M23, lina kila dalili zinazomuweka kwenye kundi la viongozi wa Kiafrika ambao hatma yao baada ya kuachia madaraka inazungukwa na wingu la mashaka.

Rais wa Marekani, Barack Obama, ambaye mapema wiki hii alikaririwa na vyombo vya habari mbalimbali duniani akimtaka Rais Kagame kuacha kukisaidia kijeshi kikundi cha waasi wa M23, anaaminika kuitoa kauli hiyo kama msimamo wa serikali yake inayopinga watawala wanaojihusisha na uhalifu wa kivita.

Ingawa hadi sasa Rais Kagame hajatajwa na Ikulu ya Marekani kama mmoja wa viongozi wa Afrika wanaotuhumiwa kwa uhalifu wa kivita, onyo lililotolewa na Rais Obama linadhihirisha kuwepo kwa ushahidi unaomhusisha na matukio ya aina hiyo yaliyopata kuwagharimu baadhi ya marais walionyooshewa kidole na Marekani kwa aina hii hii anayonyooshewa sasa Kagame.

Wadadisi na wafuatiliaji wa mambo walioichambua kauli ya Rais Obama, wanaeleza kuwa aliitoa baada ya Marekani kujiridhisha na ushahidi ilioukusanya ukiihusisha Serikali ya Rwanda kuwasaidia waasi wa kundi la M23.

Wanaeleza kuwa Marekani baada ya kubaini ushirika wa majeshi ya Rwanda yaliyojipenyeza ndani ya makundi ya waasi wanaopigana na Serikali ya Kongo, huku wakitekeleza vitendo vya kinyama dhidi ya binadamu katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa madini, imeamua kumtosa Kagame, ambaye amekuwa na uswahiba wa muda mrefu na taifa hilo.

Katika tathimini yao kuhusu uzito wa onyo la Rais Obama kwa Rais Kagame, wanaeleza kuwa hataweza kuepuka kitanzi cha mashitaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC).

Waasi wa kikundi cha M23, mbali na kuendesha mapambano dhidi ya majeshi ya Serikali ya Kongo, jambo linalopingwa na jumuiya ya kimataifa, pia wanatuhumiwa kwa ubakaji na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.

Tuhuma hizo pia zinaelekezwa kwa majeshi ya Rwanda, yanayodaiwa kushirikiana na waasi hao na ndizo zinazomuweka Rais Kagame katika hatari ya kufikishwa mahakamani na hata kuhukumiwa kama ilivyokuwa kwa aliyekuwa Rais wa Liberia, Charles Taylor, ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 50 jela baada ya kupatikana na makosa ya uhalifu wa kivita nchini Sierra Leone ambako zaidi ya watu 50,000 waliuawa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe na wengine wengi wakiachwa na ulemavu wa kudumu.

Kama inavyotokea kwa Rais Kagame sasa, kwa Taylor pia ilikuwa hivyo hivyo, pale alipokuwa akionywa na jumuiya za kimataifa na yeye kudharau maonyo hayo.

Wakati wadadisi na wachambuzi wa mambo wakiwa na mtizamo huo kuhusu onyo la Serikali ya Marekani dhidi ya Rais Kagame kujiingiza kijeshi katika vita vya ndani ya Kongo, ushahidi uliokusanywa na taasisi za Umoja ya Mataifa za kutoa misaada ya kibinadamu unaonyesha kuwa wanajeshi wa Rwanda wanaopigana bega kwa bega na waasi wa M23 wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya kihalifu dhidi ya binadamu.

Ni ushahidi wa aina hiyo ndio uliotumiwa na ICC, kumhukumu Taylor, aliyekuwa akituhumiwa kuvisaidia vikundi vya waasi vya Revolutionary United Front (RUF) na Armed Forces Revolutionary Council (AFRC) kwa kuvigawia silaha za kivita kwa muktadha wa kupewa madini ya almasi.

Stephen Rapp, mchambuzi wa sheria za makosa ya jinai wa Marekani, katika mahojiano yake na gazeti la The Guardian la nchini Uingereza, alieleza kuwa uongozi wa Serikali ya Rwanda una tuhuma za kujibu katika Mahakama ya ICC, kuhusu mapigano yanayoendelea Mashariki mwa Kongo.

Kauli hiyo ya Rapp inaunga mkono madai ya mara kwa mara ya mashirika ya kimataifa yanayojihusisha na utetezi wa haki za binadamu ya Human Right Watch, Save the Children, UNICEF na UNHCR, ambayo kwa nyakati tofauti yamekuwa yakidai kuwa na ushahidi wa kutosha wa waasi wa M23 kusaidiwa na Jeshi la Rwanda kufanya mauaji ya raia wasiokuwa na hatia katika miji mbalimbali ya Mashariki mwa Kongo.

Inadaiwa pia kuwa upo ushahidi unaoonyesha jinsi ambavyo waasi wa M23 wamekuwa wakiwatumia watoto wadogo katika vikosi vya majeshi na ndio ambao wamekuwa wakitangulizwa mstari wa mbele katika uwanja wa mapambano, hususan katika matukio ya uhalifu wa kivita.

Tuhuma nyingine zinazoelekezewa Serikali ya Kigali ni kufadhili kundi la waasi la CNDP, lililokuwa chini ya uongozi wa Jenerali Bosco Ntaganda, ambaye amejisalimisha kwenye Mahakama ya ICC mapema mwaka huu.

Sehemu kubwa ya wapiganaji wa kundi la Ntaganda sasa wameungana na waasi wa kundi la M23 na wamekuwa wakijiimarisha kiulinzi katika maeneo yenye utajiri mkubwa wa madini nchini Kongo.
Mtanzania