Pages

KILICHOJIRI MAHAKAMANI TABORA KESI YA MUME WA JOYCE KIRIA

 Chadema Tabora Kamanda Mbaruk,
Juzi nikiwa mahakamani Tabora kulia kwangu ni M/Kiti wa Chadema Tabora Kamanda Mbaruk, kushoto ni shemeji yangu Kamanda Bella.
Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuingia MAHAKAMA KUU ambapo nilishuhudia jaji akifanya kazi yake kwa busara iliyopitiliza (kwa maoni ya Wakili msomi Peter Kibatala)
Chadema Tabora
Kamanda wangu Mume wangu (kombati nyeusi) na shemeji zangu wakiingia mahakamani jana mjini Tabota.
Masuala ya Mahakamani yanaitaji subira ya hali ya juu hivyo bado naendelea kumfariji Mpenzi wangu Kilewo ya kwamba mambo haya yatapita tu. zaidi ya hapo namwombea sana.
Chadema TaboraKushoto kwangu ni kamanda wa Chadema Tabora (huyu mama) na kulia ni mke mwenzangu (mumewe yupo kesi moja na mume wangu)

Kwa maoni ya Wakili Msomi PK ni kwamba Jaji alichukulia kesi hiyo kwa uzito wake na pia akaheshimu na kuzingatia hali halisi ya Wakili, kwamba anatoka mbali Dar es salaam na hivyo akaamuru Hoja za pande zote mbili zipelekwe kimaandishi kuwaondolea usumbufu hasa wapeleka maombi ambao ni sisi tunaosafiri kila siku. Na kwa sababu hizo basi tar 30july Jaji atataja tar ya uamuzi.
Asanteni sana sana najua mpo pamoja na familia yetu

KAULI YA RAISI MH.KIKWETE KUHUSU KODI YA KADI ZA SIMU

KODI YA KADI ZA SIMU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameagiza Wizara za Serikali zinahusika na kodi na mawasiliano pamoja na makampuni ya simu za mikononi nchini kukutana mara moja kutafuta jinsi gani ya kumaliza mvutano wa kodi mpya ya kadi za simu hizo za mikononi.

Rais kikwete ametoa maelekezo hayo jioni ya leo, Jumanne, Julai 23, 2013 wakati alipokutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wawakilishi wa makampuni ya simu ya TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel katika kikao cha pamoja kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Kikwete amesema kuwa lengo kuu la mkutano huo wa pamoja kati ya Wizara hizo za Serikali na makampuni ya simu yawe ya kupendekeza jinsi gani ya kuziba pengo la Sh. Bilioni 178 ambazo zitapotea katika Bajeti iwapo kodi hiyo kwa kadi za kuongelea za simu za mikononi italazimika kufutwa na Serikali kupitia marekebisho kwenye Muswada wa Fedha wa Bajeti ya Mwaka 2013/2014.
Rais Kikwete amewaambia wawakilishi wa pande hizo mbili kuwa huwezi tena kuifuta moja kwa moja kodi hiyo bila kutafuta njia nyingine za kupata fedha za kujaza pengo hilo la Sh. Bilioni 178 ambazo tayari Bunge limezipangia matumizi.
“Nawaombeni kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani tunaweza kujaza pengo hili la Sh. Bilioni 178 endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu,” Rais Kikwete amewaambia wawakilisho hao.
Katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/2014, Serikali imeweka kodi ya Sh. 1,000/= kwa mwezi kwa kila mtumiaji simu kwa ajili ya kufanya mawasiliano kwa kutumia simu ya mkononi.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
23 Julai, 2013

MAREKANI YAIONYA RWANDA KUACHA MARA MOJA KUWASAIDIA M23

 RWANDA
(Reuters) - The United States on Tuesday called on Rwanda to end support for M23 rebels in neighboring Democratic Republic of Congo, saying there was evidence Rwandan military officials were involved. "We call upon Rwanda to immediately end any support for the M23 (and) withdraw military personnel from eastern DRC," State Department spokeswoman Jen Psaki said.
She declined to say whether Rwandan President Paul Kagame was implicated. "I wasn't speaking to Kagame himself," she added.

The call comes two days before U.S. Secretary of State John Kerry leads a special session of the United Nations Security Council on Africa's Great Lakes region
Psaki said the concerns followed a "credible body of evidence" in a recent report by Human Rights Watch that said M23 rebels in Congo were to blame for executions, rapes and forcible recruitment of men and boys while receiving support from Rwanda.  RWANDA RWANDA
M23 began taking parts of eastern Congo early last year, accusing the government of failing to honor a 2009 peace deal.
(Reporting by Lesley Wroughton; Editing by Doina Chiacu)

ASKARI POLISI WATIMULIWA CHUONI HUKO MOSHI

ASKARI POLISI Wanafunzi 117 wa Polisi, wamefukuzwa katika Chuo cha Taaluma na Mafunzo ya Polisi (MPA), kilichopo Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Waliotupiwa virago na kufutwa kwenye kozi hiyo ni wale waliopoteza sifa za kuendelea na mafunzo ya kijeshi baada ya kukutwa na makosa ya utovu wa nidhamu, utoro na matatizo ya kiafya.

Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Matanga Mbushi, ambaye ni mkuu wa chuo hicho aliliambia NIPASHE katika mahojiano maalumu kwamba, waliotimuliwa chuoni ni kati ya askari wanafunzi 3,189 waliokuwa wamesajiliwa kuanza mafunzo ya kijeshi katika chuo hicho, Oktoba 25 mwaka jana.

Kati yao askari 115 ni wale wa Polisi na askari wawili wanatoka katika Idara ya Uhamiaji iliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.

Kufukuzwa kwa wanafunzi hao , kuna akisi moja kwa moja jinsi menejimenti ya chuo hicho ilivyojipanga upya kupunguza wimbi la baadhi ya askari walioko kazini na ambao wanalipaka matope jeshi hilo kutokana na kupotoka kimaadili kwa kutaka kujinufaisha kimaslahi.

Askari hao walikuwa waungane na wenzao ambao wanatarajiwa kuhitimu mafunzo ya awali ya polisi na uhamiaji, Julai 26 mwaka huu baada ya kupatiwa mafunzo ya medani za kivita. Mgeni wa heshima atakayeshuhudia kuagwa kwa askari 3,092 ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi.

Kamishna Mbushi alisema askari hao pamoja na mambo mengine wamepatiwa mafunzo maalumu ya utunzaji wa amani ya nchi iliyopo, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), Haki za Binadamu, Masuala ya mtambuka (Cross cutting issues), Usimamizi wa majanga na Usimamizi wa kazi za Polisi.

Mafunzo mengine ni pamoja na Polisi Jamii, Sheria ya ushahidi, Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, Upelelezi wa makosa ya jinai, Usalama barabarani na stadi za kazi.

Taarifa za awali kutoka ndani ya chuo hicho, zinaeleza kuwa mahafali hayo ya Polisi yatatanguliwa na medani za kivita yatakayofanyika Julai 25 huko katika Kijiji cha Kilele-Pori, Wilaya ya Siha.
HABARI LEO

Royal Baby. Here is the Family Tree

Royal baby: Family tree

Kipanya Leo

Kipanya

Final call for artists - 31 July deadline! -Sauti za Busara

BUSARA PROMOTIONS
Are you an African musician or group? Applications for local and international artists who want to perform at the 11th edition of Sauti za Busara are open until 31st of July. The festival will be held from 13-16 February 2014. The online application form is on our website HERE or a paper version can be collected at our offices in Maisara, opposite Golf Club, in Zanzibar.
Over the past ten years we have had more than 250 groups perform, in all musical genres, always 110% live.
Note that we receive many applications each year and we take the time to review each application carefully. Please be patient as we review the applications and we will inform applicants as soon as we can after the selection committee meets in early August.
Your application must include the following:
A completed online or paper form including a short biography (max 1000 words).
One or two recent recordings (CD or DVD)
One or two photographs (JPG or paper)
Please send your recordings, photographs and any other material to our office address below:

BUSARA PROMOTIONS PO BOX 3635 STONE TOWN, ZANZIBAR, TANZANIA
Please note we will not accept applications and application materials after 31 July. Make sure we have received your full application (including hard copies of recordings) by that date.
 For more information see www.busaramusic.org/callforartists

Dj Choches/tecdjs -Bongomania 5 (Audio Mixing)

Dj Choches/tecdjs,Bongomania 5, ,Audio Mixing

TMK Wanaume Family - Tunafurahi (Audio)

MJANE ALIYEFUKUZWA KATIKA MSIBA WA MWANAJESHI WA JWTZ AJITOSA TENA KUHUDHURIA MAZISHI

FAMILIA ya Marehemu, Fortunatus Msofe, ambaye ni mmoja wa wapiganaji wa JWTZ, waliofia Darfur, wamemzuia aliyekuwa mchumba wake Amina Juma kushiriki katika mazishi na kumfungia mlango wa nyumba ya marehemu asiingie ndani mara tu baada ya taarifa za kifo cha marehemu kuwafikia.
Hata hivyo Amina amelazimika kwenda Tanga kushiriki shuguli za mazishi ya marehemu pamoja na kwamba familia ya marehemu haitaki kumuona katika msiba huo.
JWTZ
Akizungumza na gazeti moja la kilasiku la kiswahili nchini Tanzania, Amina alisema kwamba ingawa awali alikata tamaa ya kumzika mwenzake, lakini jana aliamua kwenda Tanga kuhudhuria mazishi na kwamba hatua hiyo ilikuja baada ya kujishauri sana.

Baba wa marehemu, Wilbad Msofe aliiambia gazeti hilo kutoka Kange, Tanga kuwa alishangazwa na hatua ya Amina kutowafahamisha kuhusu msiba huo. Alisema hiyo ndiyo sababu za yeye kuamua kutaka mwanawe apelekwe Kange kwa mazishi.

Akizungumza na gazeti hilo akiwa njiani kwenda Kange, Amina alisema: “Nilikuwa ninataka sana kumzika mwenzangu lakini ile hali ilikuwa imenichanganya pamoja na kwamba nilishauriwa, sasa nimekata shauri nakwenda Tanga.

“Najua kuna kitu hapa, lakini ‘Fortu’ kwa kuwa nilikuwa naye, na wana ndugu wa upande wa wake wameshanikana, mimi nitamzika tu mwenzangu na kurudi,” alisisitiza.

Miili ya wapiganaji hao iliagwa jana katika Makao Makuu ya Jeshi, yaliyoko Upanga na Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange, makamanda na wanajeshi walishiriki kuwaaga wanajeshi hao.

Akizungumza kwa masikitiko na huku sauti ikiwa imemkauka kutokana na kulia muda mrefu, Amina alisema: “Siwazii mtafaruku uliopo, moyo umenituma kwenda kumzika mume wangu, niliwaza usiku kucha na leo (jana) Jumatatu asubuhi nikaamua kwenda Tanga.”

“Msofe amekufa tulikuwa tuna mipango mingi, tulipanga harusi kubwa lakini haikuwahi kufanyika, niliongea naye alfajiri ya Jumamosi ya Julai 13, akaniambia tutaongea baadaye maana wanakwenda kwenye operesheni...

“Unajua tuliishi maisha ya kipekee sana tulipendana kiukweli hata majirani tuliokuwa tukiishi nao Mbezi na Visiga wanajua hilo na wengi walikuwa wakinisihi sana nisije kumuudhi huyu kijana.

"Nafsi inauma sana. Nawashangaa wazazi wake kwa kunikana"