Pages

Blog Zote za Tanzania Zinapatikana Ndani ya Blog Moja (Directory) - Bongo Blogs

Tanzania Directory 
Acha kuzunguka blog kibao bila kupata habari uliyokua unaitafuta,  Blog ni moja tu Bongo Blogs ndio unatakiwa kukumbuka halafu nyinginezo zooote utazipata ndani yake (Bongo Blogs) bofya link..
 >> Bongo Blogs
 http://bongoblogs.blogspot.com
Blog yako ya Taifa

Unaikumbuka Ishu ya K-yline na Mzee Reginald Mengi? Cheki Picha na Mapacha Wao

 K- yline na Mzee Reginald Mengi

Tanzania's Hadzabe. Bushman at the Lake Eyasi (Video)

The Hadza, or Hadzabe, are an ethnic group in north-central Tanzania, living around Lake Eyasi in the central Rift Valley and in the neighboring Serengeti Plateau. The Hadza number just under 1000. Some 300--400 Hadza live as hunter-gatherers, much as their ancestors have for thousands or even tens of thousands of years; they are the last full-time hunter-gatherers in Africa.

STARS YALAZWA 1-0 NA UGANDA, HASHEEM THABEET wa NBA AWA KIVUTIO KIKUBWA KWA MASHABIKI UWANJANI

 Thunder,
Mtanzania anayecheza kikapu katika Ligi ya Marekani maarufu kama NBA, Hasheem Thabeet, amekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa soka kwenye Uwanja wa Taifa,Dar.

Thabeet anayecheza katika timu ya Thunder, aliibuka na kuwasalimia mashabiki wakati Taifa Stars ikivaa Uganda nao walimshangilia kwa nguvu sana.
 NBA, Hasheem Thabeet

 NBA, Hasheem Thabeet
BAO pekee la Dennis Iguma dakika ya 46 jioni hii limeiwezesha Uganda kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye michuano ya Ubingwa wa Mataifa wa Mataifa Afrika (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.

Amri Kiemba akipasua ngome ya Uganda katika mchezo wa leo Uwanjqa wa Taifa, Dar es Salaam.

Iguma aliifungia The Cranes bao hilo, baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Stars kufuatia krosi maridadi ya Brian Majwega, ambaye leo alikuwa mwiba mkali kwa Taifa Stars.

Hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na kwa ujumla katika dakika zote hizo 45 hakukuwa na shambulizi la kutisha kwa pande zote.

Brian Majwega alifanikiwa kumgeuza uchochoro Erasto Nyoni na kuingia ndani mara kadhaa, lakini pasi na krosi zake ziliokolewa na mabeki wa Stars inayofundishwa na Mdenmark, Kim Poulsen.

Mrisho Ngassa alipewa mipira mirefu kadhaa, lakini mabeki wa Uganda wakiongozwa na mkongwe, Nahodha wao, Hassan Wasswa walisimama imara kumdhibiti.

Mashambulizi mengine ya Stars yalipitia kwa John Bocco ‘Adebayor’, ambaye alikuwa anapigiwa mipira mirefu, lakini alidhibitiwa pia. Timu zote zilicheza sawa kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko, Stars ikiwapumzisha beki Erasto Nyoni na kiungo Mwinyi Kazimoto na kuwaingiza David Luhende na Haroun Chanongo, lakini walikuwa ni Uganda wanaofundishwa na makocha wa zamani wa klabu ya Yanga, Mserbia Milutin Sredojevic ‘Micho’ anayesaidiwa na Sam Timbe waliobuka vinara.

Lakini baada ya kufungwa Stars, waliongeza kasi na nguvu ya uchezaji na kufanikiwa tu kulitia misukosuko lango la Uganda na si kupata bao japo la kusawazisha.

Matokeo hayo yanamaanisha Stars itahitaji kushinda ugenini kuanzia mabao 2-0 wiki mbili zijazo ili isonge mbele, vinginevyo itakuwa imetupwa nje ya mashindano hayo.

Katika mchezo wa leo kikosi cha Stars kilikuwa; Taifa Stars; Juma Kaseja, Erasto Nyoni/David Luhende, Shomary Kapombe, Aggrey Morris, Kevin Yondan, Frank Domayo, Amri Kiemba, Salum Abubakar, John Bocco ‘Adebayor’, Mwinyi Kazimoto/Haruna Chanongo na Mrisho Ngassa.

The Cranes; Hamza Muwonge, Hassan Wasswa, Nico Wadada, Brian Majwega, Savio Kabugo, Richard Kasaga, Dennis Iguma, Said Kyeyune, Joseph Mpanda, Patrick Edema/Ivan Ntege na Tonny Odur/Frank Kalanda.
Mrisho Ngassa
Mshambuliaji wa timu ya Taifa (Taifa Stars),John Boko (14) akiwa na mpira mbele ya Beki wa timu ya Uganda ( The Cranes) katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Kombe la mashindano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN),uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa Stars imekubali kipigo cha Bao 1-0 kutoka kwa Uganda.
Mrisho Ngassa
Mrisho Ngassa
Mrisho Ngassa akitaka kuwatoka Mabeki wa Uganda wakati wa mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Kombe la mashindano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN),uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa Stars imekubali kipigo cha Bao 1-0 kutoka kwa Uganda. Mrisho Ngassa
Mrisho Ngassa Mdodosaji

JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA LITAADHIMISHA SIKU YA MASHUJAA MKOANI KAGERA

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
11 Julai, 2013
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linaadhimisha siku ya mashujaa kila tarehe 25 Julai, ikiwa ni sehemu ya kuwakumbuka mashujaa waliopigana na kushinda vita ya Kagera mwaka 1978/1979.

Maadhimisho hayo hufanyika mara moja kwa mwaka, na mwaka huu yatafanyika tarehe 25 Julai 2013 katika mkoa wa Kagera wilaya ya Bukoba kwenye makaburi ya mashujaa yaliyopo Kaboya.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. JAKAYA MRISHO KIKWETE.

Sambamba na mgeni rasmi, watakuwepo viongozi waandamizi wa Serikali, vyombo vya Ulinzi na Usalama, vyama vya siasa, taasisi za dini na taasisi mbalimbali za kiraia.

Vyombo vya habari vinaalikwa kushiriki katika maadhimisho hayo ambayo ni muhimu kwa Taifa.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0764742161
Email: ulinzimagazine@yahoo.co.uk

WATOTO SABA WAMENUSURIKA KUUZWA

 Burundi na Rwanda Watoto saba ambao ni raia wa Burundi na Rwanda ambao walikamatwa wakati walipokuwa wakisafirishwa kutoka Burundi kuja Tabora kwa ajili ya kuuzwa

watumikishwe katika mashamba ya tumbaku,Watoto hawa walikamatwa eneo la Ulyankulu wilayani Kaliua wakiwa na tajiri yao ambaye amefahamika kwa jina la Emmanuel John(22) ambaye pia ni raia wa Burundi.
Watoto wakiwa mahakama ya hakimu mkazi Tabora wakisubiri kuingia mahakamani kutoa ushahidi baada ya mtu aliyekuwa amewasafirisha kwa lengo la kutaka kuwauza kukamatwa na kufikishwa Mahakamani kujibu shitaka la kuwasafirisha kwa nia ya kuwafanyia biashara na kuingia nchini kinyume cha sheria.

Afisa na Mwanasheria wa Idara ya Uhamiaji mkoa wa Tabora akiwaongoza watoto hao kuingia chumba cha mahakama ya hakimu mkazi Tabora kwa ajili ya kutoa ushahidi dhidi ya Emmanuel John.

RAIA wa Burundi, Emmanuel John (22),aliyekamatwa akituhumiwa kusafirisha watoto,amefikishwa katika Mahakama ya Mkoa waTabora akikabiliwa na Mashitaka mawili moja likiwa ni la kuingia nchini kinyume cha sheria na kusafirisha binadamu kwa lengo la kutaka kuwauza.
 Burundi na Rwanda
Mbele ya Hakimu Mkazi Bw. Jackton Rushwela,Wakili wa Serikali Bw.Iddi Mgeni, alimsomea mshitakiwa mashitaka hayo ambapo alikiri kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria huku kosa la pili la kuwasafirisha watoto hao saba akijaribu kutaka kuficha ukweli.

Kutokana na kukiri kosa la kwanza, Hakimu Rushwela alimhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya sh 100,000.

Hata hivyo,mshitakiwa huyo Emmanuel John pamoja na kuiomba mahakama impatie fursa ya kumtaarifu mkewe aliyeko huko nyumbani kwao nchini Burundi kwa njia ya simu au apewe nafasi ya kuuza simu yake ya mkononi aweze kulipa faini hiyo kwa nia ya kutaka kujinasua na adhabu ya kifungo hicho cha mwaka mmoja lakini mahakama haikuwa tayari kutekeleza hilo.
 Burundi na Rwanda
Kuhusu shitaka la kusafirisha binadamu,upande wa mashitaka ulidai mshtakiwa alikamatwa na maofisa wa Idara ya Uhamiaji akiwasafirisha watoto Ndayisenga Batiliza(13), Ndakusenga Emmanuel(15), Nimbonajile Nagenda(13), Yazid John(15), James Justus(14) na Samson Banteke(17).

Baadhi ya watoto hao walitoa ushahidi walidai walisafirishwa na mshitakiwa Emmanuel John kutoka nchini Burundi na Rwanda hadi walipokamatwa eneo la Ulyankulu wilayani Kaliua.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 25, mwaka huu itakapoendelea tena kusikilizwa kwa mashahidi wengine kutoa ushahidi wao.

Emirates Hosts Iftar Celebrations in Tanzania

Tanzania Abdulaziz Al HaiEmirates Country Manager for Tanzania Abdulaziz Al Hai speaking to the Media during the Iftar dinner last evening in honour of its trade partners and the Media at the Hyatt Regency Dar es Salaam, the Kilimanjaro.

Emirates, one of the world’s fastest growing airlines, hosted Iftardinner last evening in honour of its trade partners and the media at the Marquee Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kiimanjaro.

Speaking at the event, Emirates Country Manager for Tanzania Abdulaziz Al Hai thanked the Government of Tanzania, trade partners and the media for their outstanding and continuous support to the airline.
“Ramadan is a period of sharing and we are pleased that each one of you found time to join us as we celebrate Iftar,” said Al Hai. “Our services in Tanzania have gone from strength to strength over the last 15 years and we owe our success to the very important partnerships we have with our trade partners, our loyal customers, as well as the media. This event is an amicable opportunity for us to show our appreciation for your vital role in the growth of Emirates in Tanzania. I am confident we can always count on your assistance going forward.”

He noted that the provision of excellent in-flight service and entertainment, ongoing network expansion and focus on developing innovative ways to improve customer comfort and convenience have been key in driving success for Emirates in Tanzania.

“Our modern and convenient Dubai hub enables our customers to seamlessly connect to our ever-expanding global network,” Al Hai said.

Emirates established operations in Tanzania in 1997. Currently, the airline flies daily from Julius Nyerere International Airport (JNIA) to Dubai, connecting passengers to 134 destinations in 77 countries across six continents.

EK 725 departs Dubai International Airport every day at 1015hrs and arrives at the Julius Nyerere International Airport (JNIA) in Dar es Salaam at 1455hrs. The return flight leaves JNIA at 1645hrs and lands in Dubai at 2320hrs every day.
More information on offering conditions and bookings can be obtained from www.emirates.com/tz

KWA WANAUME WOTE: MASANJA MKANDAMIZAJI

 MASANJA MKANDAMIZAJI
Mwanaume kuwa na hela ni sawa na Mwanamke kuwa mzuri,hela kwa Mwanaume ni dalili wewe ni Fighter,ni hard-worker,ni Success Chaser,ni Paper finder..hizi ndo aina za watu Wanawake wanataka...Sio maneno mengi unanukia Pafyumu kama muuza urembo wa Buguruni, hela huna,ur simply useless man,hupati mtu...Fanya kazi kwa bidii,mafanikio -hayaji kwa kushinda Bar na kuuza Sura Samaki -Samaki.
Hela huna na Sura huna,sasa tukusaidiaje?

Uhuru Kenyatta on Churchill Live

Mama Ntilie Jijini Dar Wanatumika Kuuza Dawa za Kulevya

Mama Ntilie Dar es Salaam. Biashara ya dawa za kulevya nchini inazidi kuchukua sura mpya ambapo sasa wanawake wanaouza vyakula, maarufu mama ntilie, hutumika kusambaza dawa hizo kwa wateja.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa muda mrefu katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam unaonyesha kuwa biashara hiyo inafanyika katika maeneo ya Tandika, Manzese, Vingunguti, Temeke, Tandale, Mtongani na Keko.
Wanawake hao wamekuwa wakitumia mwanya wa kuuza chakula kama kinga yao, huku biashara yao kubwa ikiwa ni kuuza dawa za kulevya aina ya heroin, bangi na aina nyingine.

Mbinu hii mpya ya usambazaji wa dawa za kulevya kwa kutumia wanawake wanaouza vyakula imeelezwa kuwa inawasaidia wahusika wakuu, kuendesha biashara yao kwa ufanisi zaidi.

Uchunguzi umeonyesha kuwa wafanyabiashara wa dawa hizo wameamua kuwatumia mamalishe kutokana na kuwa waaminifu na kuhudumia wateja wengi, hivyo ni vigumu watu kuwashtukia wakiwamo askari polisi.

Imebainika kuwa dawa hizo huuzwa kulingana na maeneo, wakati maeneo ya watu wasiokuwa wa uwezo hupimwa kwa kutumia kipimo kidogo zaidi kwa bei ya chini ambayo watumiaji husika huweza kuimudu.

Aidha dawa hizo hufungwa katika mitindo miwili tofauti, ukiwa katika unga wa vidonge na wa kawaida ingawa bei zake hazitofautiani sana.

Uchunguzi unaonyesha kuwa vidoge huuzwa vikiwa vizima au vipande, huku unga wa kawaida ukiuzwa kwa kipimo maalumu.

Kwa kawaida ‘unga’ huo huuzwa kwa Sh1,000 kwa pointi huku kete moja ikiuzwa kwa Sh2,000, wakati vidonge, kizima huuzwa kwa Sh2,000, huku kipande huuzwa kwa Sh1,000 zikitofautiana kulingana na maeneo.

Gazeti hili lilifanikiwa kuongea na baadhi ya wanawake wanaojihusisha na uuzaji wa dawa hizo.

Dada mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Asha (28) ambaye siyo jina lake halisi ni muuzaji mkubwa wa dawa hizo. Awali alikuwa akifanya shughuli zake hizo za uuzaji katika maeneo ya Yombo Kilakala, ingawaje hivi sasa amehamia Temeke.

“Unajua siku zote dhumuni la kufanya biashara ni kupata faida, hivyo naweza kusema niliingia kwenye biashara hii kwa sababu tu ina faida zaidi kuliko biashara nyingine,” anasema.

Awali alikuwa akiuza vyakula huku akifanya biashara hiyo ya kuuza dawa, baadaye akaacha kuuza vyakula akabaki na biashara ya dawa za kulevya.

Akielezea namna anavyofanya biashara yake hiyo, Asha anasema kwa kawaida huwa ananunua mkanda ambao unakuwa umefungwa vidoge vidogovidogo kumi hadi ishirini. Mara nyingi huuza kulingana na mahitaji ya mteja.
“Halafu baada ya kununua hivyo huwa nauza kidogokidogo vidonge hivyo.

Kwa kawaida kidoge kimoja huwa nauza kati ya sh1,000 hadi Sh2,000. Bei yake hutegemea na mahali unapouzia. Kama unauzia watu waliochoka sana inabidi upaki kidogokidogo ili kuweza kuliteka soko lao,” anasema.
“Nimefanya biashara hii kwa muda wa miaka mitatu, lakini ukweli ni kwamba hadi sasa nimefanikiwa kwa kiasi fulani. Nimeweza kujenga nyumba ya kwangu mwenyewe, pia kuhudumia familia yangu. Licha ya kuwa na madhara kwa watu, lakini ukweli ni kuwa biashara ya unga inalipa,” anasisitiza.

Abubakari Ismail (33) aliyewahi kutumia dawa za kulevya, ambaye kwa sasa ni kiongozi wa kupambana na dawa hizo kinachofahamika kama Use Ant -Drugs, kilichopo Yombo, wilayani Temeke, anasema kuwa tatizo la wanawake kujihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya linachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha mapambano dhidi ya dawa hizo hususan kwa vijana.

‘Joseph (17)’, siyo jina lake halisi ni kijana aliyekuwa katika matibabu kutokana na matumizi ya dawa za kulevya. Hivi sasa kijana huyu amelazimika kuhama nyumbani kwao kutokana na kumkimbia mama yake mzazi ambaye anajihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya.

Mkurugenzi wa Kituo cha Makangarawe Youth Information Center cha jijini Dar es Salaam, kinachojishughulisha na miradi kadhaa ya vijana ikiwamo mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa vijana, Ismail Mnikite, amesema kitendo cha wanawake kushiriki katika uuzaji wa dawa za kulevya ni tatizo jipya linalochangia kukwamisha juhudi za mapambano hayo.
Mwananchi