Pages

Chris Brown Faces Prison

Chris Brown
Chris Brown is facing up to a year in prison after being charged following an alleged hit-and-run in Los Angeles.
The LA city attorney’s office has also charged the singer with driving without a valid licence.
A spokesman said the charge related to a minor accident on May 21 in the San Fernando Valley.
It is not up to the county district attorney’s office and the courts to determine if the case will have any effect on Brown’s felony probation in the 2009 beating of singer Rihanna.
Brown pleaded guilty to felony assault of his then-girlfriend and was sentenced to five years of probation and six months of community service.

Lange ft Soprano - Naongea Nawewe (Video)

Lange ft Soprano - Naongea Nawewe

TFF Kuendesha Kozi Sita Tofauti

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFFNa Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaendesha kozi sita tofauti za mpira wa miguu kati ya Julai na Septemba mwaka huu.
Kozi hizo ni FIFA 11 For Health itakayofanyika Hombolo mkoani Dodoma kuanzia Julai 8 hadi 19 mwaka huu. Julai 6 hadi 15 mwaka huu kutakuwa na kozi ya mpira wa miguu wa ufukweni (Beach Soccer) itakayofanyika jijini Dar es Salaam.
Waamuzi wa FIFA nao watakuwa na kozi itakayofanyika kati ya Agosti 22 hadi 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati kozi ya ukocha kwa ajili ya Copa Coca-Cola itafanyika jijini Dar es Salaam kati ya Agosti 12 na 17 mwaka huu.
Vilevile kutakuwa na kozi ya mpango wa grassroots unaolenga wachezaji mpira wa miguu (wasichana na wavulana) wenye umri kuanzia miaka 6-12 itafanyika kuanzia Septemba 9 hadi 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati tamasha (festival) la grassroots litafanyika Uwanja wa Karume, Septemba 14 mwaka huu.

CUF Wameaahirisha Maandamano ya Kwenda Ikulu

CUFNaibu Katibu Mkuu wa CUF Julius Mtatiro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,kuhusu maandamano ya kupeleka kilio cha wana Mtwara Ikulu,ambapo yameahirishwa kupisha ujio wa Rais wa Marekani Barrack Obama,kushoto ni Ofisa Chama hicho Mikidadi Ibrahimu.Picha na Michael Jamson

Dar es Salaaam. Chama cha Wananchi (CUF) kimeahirisha maandamano yaliyopangwa kufanyika Juni 29 mwaka huu kwa sababu Rais Jakaya Kikwete, atakuwa katika Mkutano wa Kimataifa wa Smart Partnership na kushughulikia ziara ya Rais Barack Obama wa Marekani.

Maandamano hayo yalikuwa na lengo la kumfikishia Rais Kikwete ujumbe kuhusu vitendo vya ukatili, wizi, ubakaji na mauaji vinavyofanywa na polisi mkoani Mtwara na kutaka uchunguzi kuhusu matukio ya Arusha.

Hata hivyo kuahirishwa kwa maandamano hayo kunakuja baada ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova kupiga marufuku maandamano ya aina yoyote na kwamba polisi watapambana na yeyote atakayakaidi amri hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema: “Tumepokea barua kutoka Ikulu, kutuomba tusitishe maandamano hayo kwa sababu Rais ambaye ndiye mpokeaji wa maandamano hayo atapokea wageni mbalimbali watakaoingia nchini,” alidai.

Mtatiro alisema barua hiyo ilieleza kuwa haitawezekana Rais kupokea maandamano ya CUF kwa kuwa atakuwa akipokea wageni mbalimbali.

“Sisi tulimwandikia Rais barua kuwa Juni 29 mwaka huu tutakuwa na maandamano ya kuelekea Ikulu,hatukujua kama kutakuwa na ugeni wa marais siku hiyo...tumeahirisha,”alisema.
Mwananchi

KUPINGA KAULI YA WAZIRI MKUU "Wapigwe tu" ALIYOITOA BUNGENI TAREHE 20/06/2013 -Legal and Human Right Center

Taarifa hii ni matokeo ya ufuatiliaji wa utendaji wa shughuli za Serikali kama zinavyowasilishwa bungeni na kauli ya Waziri Mkuu (Mtendaji Mkuu wa shughuli za serikali Bungeni) aliyoitoa, Alhamisi ya tarehe 20 Juni 2013, wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo. Waziri Mkuu Pinda, alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama, hususan Jeshi la Polisi kuwapiga wananchi watakao kaidi na kupinga amri halali ya jeshi hilo.

Katika tamko hilo, Pinda alisema Serikali imechoshwa na vurugu na kwamba hakuna namna nyingine ya kupambana na wananchi wanaodharau vyombo vya dola zaidi ya kipigo.

Waziri Mkuu Pinda alitoa msimamo huo Bungeni, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM), aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na Serikali kufuatia kuwa na matukio ya vurugu ya mara kwa mara nchini, hususan huko Mtwara na Arusha.

Katika majibu yake, Mh. Pinda, pamoja na mambo mengine alisema kuwa; “Mheshimiwa Mangungu hapa ameanza vizuri, lakini mwisho hapa naona anasema vyombo vya dola vinapiga watu, ukifanya fujo au umeambiwa usifanye hiki ukaamua kukaidi utapigwa tu.

Akaendelea kusema kuwa, “Lazima wote tukubaliane kuwa nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya sheria na kama wewe umekaidi, unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndio jeuri zaidi, watakupiga tu.

“Na mimi nasema wanaokaidi amri halali ya Jeshi la Polisi muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine ya kupambana na wakaidi zaidi ya kuwapiga,” alisema Pinda.

Ndugu wanahabari, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimepokea kwa mshituko kauli hii iliyotolewa na kiongozi wa juu serikalini.

Maudhui ya kauli hii ni kinyume kabisa cha Katiba ,Sheria za nchi na misingi ya haki za binadamu. katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi ya ukiukwaji wa haki za binadamu hasa yale yanayotokana na vyombo vya dola na jeshi la polisi nchini, ambapo jeshi la polisi limekuwa likitumia nguvu kubwa kupita kiasi katika matukio mbali mbali na kusababisha vifo na kujeruhi watu na hata watu ambao hawakukiuka amri halali ya jeshi hilo.

Matukio haya ya matumizi makubwa ya nguvu za dola ni kinyume na taratibu za utekelezaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 13 (1) Usawa mbele ya sheria , (3)” Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya watu yatalindwa na kuamuliwa na Mahakama na vyombo vingine vya mamlaka ya nchi vilivyowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria” na (6) (b) ambayo inasema ni “Ni marufuku kwa mtu ………….kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka atakapo thibitika kuwa anayohatia ya kutenda kosa hilo” (e) Ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazo mtweza au kumdhalilisha.”

Pia ni Kinyume na kifungu namba 21 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai inayounda sura namba 20 ya sheria za Tanzania inayozuia matumizi ya nguvu kupita kiasi na kifungu namba 46 cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma saidizi “Police force and auxiliary Act” Sura namba 322 kama zilivyorekebishwa mwaka 2002, ambayo inaelekeza kukamatwa kwa mtu aliyetenda kosa na si kupigwa. Matumizi makubwa ya nguvu pia ni kinyume na Mikataba ya kimataifa iliyoridhiwa na Tanzania na inayotambuliwa kwenye Katiba kama Tamko la Haki za Binadamu la Mwaka 1948 na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa wa Mwaka 1966.
Helen Kijo-BisimbaMkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Haki za Binadamu cha (Legal and Human Right Center) Daktari Helen Kijo-Bisimba (Kulia)

Tungependa kumkumbusha Mheshimiwa Waziri Mkuu kuwa Utawala wa sheria unajumuisha serikali, na vyombo vya utekelezaji na ulinzi pamoja na wananchi kuheshimu sheria. Na sio kuvunja sheria kwa vyombo vya usimamizi wa sheria.

Tamko hili la Waziri Mkuu limetoa mwanya mkubwa na a nguvu kwa vyombo vya usimamizi wa sheria kuvunja haki za raia. Ikumbwe kuwa yapo matukio mengi ya polisi kutumia vibaya nafasi yao na nguvu waliyonayo katika kuwavunjia haki wananchi kama mauaji yaliyofanywa huko Songea mwezi wa Pili mwaka 2012 ambapo watu wawili waliuwawa na polisi na wengine 48 kujeruhiwa, Iringa mwezi wa tisa 2012 ambapo mtu mmoja aliuwawa (Daudi Mwangosya), Tabora - Usinge 2011 ambapo mtu mmoja aliuwawa. Haya ni baadhi tu ya matokeo ya matumizi makubwa ya nguvu ya polisi.

Pamoja na hayo yapo matukio ya polisi kuuwa raia na kuwajeruhi kwenye matukio tofauti tofauti hapa nchini ambayo mpaka sasa Kituo kina matukio ya watu 11 ambao wameuwawa mikononi mwa polisi. Haya yote yanatokea kwa sababu jeshi la polisi limeshindwa kufanya kazi zake kwa kuzingatia sheria na pia kutambua wajibu wao kwa wananchi.

Katika hali hii ya kushtusha, kwenye nchi yenye Amani na Utulivu na kama tunavyopenda kusema kisiwa cha amani, kiongozi huyu wa ngazi za juu anatoa tamko linaloashiria kutoa ruksa kwa Jeshi la polisi kuvunja sheria tena tamko linatolewa hadharani, mbele ya chombo kinachoheshimika kama Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tofauti na misingi ya Katiba na Haki za Binadamu ni hatari kwa amani na utulivi huo. . Waziri Mkuu anapaswa kuheshimu na kuilinda katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria za nchi na kuhakikisha usalama wa raia.

Hivyo basi Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa kushirikiana na Watanzania wanaopenda heshima ya sheria na haki za binadamu na asasi za kiraia tumeendaa waraka unaokusanya saini za watanzania zikimtaka Mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda;

1. Kwanza kabisa kufuta kauli yake aliyoitoa bungeni kubariki polisi kupiga raia katika Mkutano huu wa Bunge la Bajeti.
2. Kuwaomba radhi Watanzania kwa kile alichosema bungeni.
3. Kulielekeza jeshi la polisi kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizoko katika kutekeleza kazi zake za kulinda usalama wa raia na mali zao.

Mpaka sasa tumeshakusanya saini 1000 kudai kauli hii ifutwe ilikulinda maisha ya Watanzania.
Imetolewa kwa Ushirikiano wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu leo Tarehe 26/06/2013.__________________
Daktari Helen Kijo-Bisimba
Mkurugenzi Mtendaji

UCHAGUZI BFT JULAI 7:TANZANIA BOXING

TANZANIA BOXING TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Yah:- Uchaguzi wa viongozi wa BFT.
Uchaguzi wa viongozi wa BFT uliopangwa Kufanyika tarehe 7/7/2013 jijini Mwanza, utafanyika kwa tarehe hiyo kama ulivyopangwa.
Kikao cha kamati ya utendaji ya BFT kilichofanyika juzi katika ofisi za BFT kikiongozwa na Rais wa shirikisho Joan Minja kimesisitiza kuwa uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa na haujaairishwa kama baadhi ya kikundi cha watu wachache wanaojiita wadau wanavyoweka pingamizi na kupotosha kwa kuwashawishi wajumbe wa mkutanao mkuu hasa kutoka mikoani kutohudhuria mkutano huo wa uchaguzi,kwa manufaa yao binafsi na kinyume na katiba yetu.
Upotoshaji huo unafanywa na Akaroly Godfrey aliyekuwa kiongozi katika uongozi uliojiudhuru kutokana na kashfa za kusafirisha madawa ya kulevya na kusababisha Tanzania kufutwa uanachama na chama cha ngumi cha dunia (AIBA) na kusababisha kutoshiriki mashindano,mikutano na shughuri zote za kimataifa za chama cha ngumi cha Dunia AIBA. Naomba wadau na serikali kuwa makini na watu wanaoshawishi kwa lengo la masilahi yao binafsi na kusababisha michezo kudolola badala ya kusonga mbele.

Fomu za uchaguzi zilishaanza kutolewa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) toka tarehe 4//2013 na zitaendelea kutolewa hadi tarehe 4/7/2013 jijini Mwanza na tarehe hiyo ndio itakuwa siku ya mwisho ya kuchukua na kurudisha fomu, tarehe 5/7/2013 itatakuwa siku ya usaili na utafanyika jijini mwanza, tarehe 6/7/2013 kupitia pingamizi na kuzitolea maamuzi na tarehe 7/7/2013 ndio siku ya uchaguzi.

Kimsingi taratibu zote za kuitisha uchaguzi kwa mujibu wa katiba yetu zimezingatiwa na zimekamilika.

Aidha BFT inatoa tamko kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufika katika uchaguzi uchaguzi, ili kupata viongozi halali kwa mujibu wa katiba, waendelee na shughuri za kuendeleza mchezo wa ndondi na kuaandaa timu ya taifa kushiriki katika mashindano ya Afrika nchini Mauritius Sept. 2013

BFT inatoa wito kwa watu wote wenye sifa, nia, moyo na uwezo wa kuongoza wajitokeze kuchukua fomu za kugombea uongozi kwani wakati ndio huu.
Makore Mashaga
Katibu Mkuu.

Yeah! That's Kanye Na Kim Kardashian wIth Baby North (Photos)

Kanye,Kim,Baby North, Baby, North Baby NorthKanye,Kim,Baby North, Baby, NorthKanye,Kim,Baby North, Baby, NorthKanye,Kim,Baby North, Baby, North

Mwisho Mwampamba Amefungua Duka la Toy la Watoto Sinza Palestina

Mwisho Mwampamba 
Mwisho Mwampamba mshiriki wa Big Brother ya kwanza kabisa baada ya kimya kingi chakuweka makazi pande za Namibia yeye na familia yake, sasa hivi amerudi nyumbani na amekuja kikazi zaidi na kuamua kufungua duka la toy za watoto lenye kila kitu ambavyo mtoto atachezea. Duka hili lipo maeneo ya Sinza Palestina linatizamana na msikiti mkuu. Sinza PalestinaMwisho Mwampamba

Maroon 5 -One More Night (Video)

Border Wars: Meth Mobile (Documentary)

Drug smuggling has reached Texas-sized proportions in the Rio Grande Valley. A canine unit detects a suspicious vehicle coming in from Mexico, and agents discover a massive quantity of methamphetamine concealed within. Within walking distance of the Mexican border, Brownsville PD and Border Patrol K-9 units discover a suspicious-looking vehicle awaiting export into Mexico, and are shocked to uncover an entire payload containing thousands of rounds of ammunition and weapons.