Pages

SOMA KILICHOMFUKUZISHA KASEJA SIMBA SC

Sports Lady PAMOJA na kutowekwa wazi sababu rasmi ya kuachwa kwa kipa Juma Kaseja, imebainika kwamba ni kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya mahasimu wao Yanga.
Simba ilipokea kipigo hicho, katika mchezo wa funga dimba wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Mei 18 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Kaseja Ndiye aliyekaa langoni.
Sports Lady Blog imezinyaka habari za kuaminika toka ndani ya uongozi wa Simba zinaeleza kwamba, kitendo kile kimewaudhi sana viongozi kwani mabao aliyofungwa yalionbekana dhahiri kuwa yalitokana na uzembe wake.
Kiongozi mmoja wa Simba aliliambia gazeti hili kwamba, pamoja na mapungufu yote aliyonayo Kaseja lakini walikerwa zaidi na kufungwa kwake.
“Hivi unavyomfahamu wewe Kaseja anaseweza kufungwa mabao kama yale, kwa kweli hilo limetacha na maswali mengi kichwani, imetkera sana mwache aende zake,”alisema
Akienda mbali zaidi, kiongozi huyo ingekuwa vizuri zaidi kama Kaseja angeweza kuonesha umahiri wake na kuondoa dhana mbovu dhidi yake, lakini kitendo cha kukubali nyavu zake kutikiswa kilitoa jawabu juu ya maswali walitokuwa nayo.
Hivi karibuni kumekuwa na utata juu ya Kaseja kusajiliwa tena kwenye kikosi cha Simba baada ya mkataba wake kumalizika huku baadhi wakitaka aongezwe na wengine wakipinga.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa klabu hiyo Alhaj Ismail Aden Rage, Kaimu Makamu Joseph Itang’are ‘Kinesi’ na Mwenyekiti wa kamati ya usajili, zakaria Hanspoppe kwa nyakati tofauti walisema Kaseja hawezi kuongezwa mkataba.
Viongozi hao walitoa kauli hizo bila ya kueleza wazi sababu za kumuacha kipa huyo namba moja wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ambaye ameitumikia klabu hiyo karibu miaka 10.
Huku hayo yakiendelea, Kaseja mwenyewe ameendeklea kukaa kimya na hata alipotafutwa kuzungumzia hilo hakuwa tayari.
 Na Dina Ismail

Bath Salts -Causing 'Excited Delirium' 'Zombie'?


Wafanya Biashara Ndogondogo Waondolewa Maeneo Mbalimbali Jijini Dar es Salaam.

Kutokana na ujio wa rais Obama nchini pamoja na viongozi wengine wa kimataifa,ITV imezunguka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar Es Salaam na kushuhudia zoezi la kuwaondoa wafanyabishara wadogodogo likiendelea chini ya usimamizi wa jeshi la polisi ikiwemo eneo la Ubungo ambapo rais Obama anatarajiwa kufanya ziara yake ya pili katika mtambo wa umeme wa Symbion power.

KIDD KIDD "HAPPY SAD" Prod by Nascent & Qb (Video)

Mbunge ‘Sugu’ afikishwa Mahakamani na Kushinda Kesi ya Kumuita Waziri Mkuu ‘Mpumbavu’

 Joseph Mbilinyi Leo asubuhi Joseph Mbilinyi (Sugu) alipelekwa mahakamani kwa shitaka la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Waziri Mkuu, shtaka hili lilifunguliwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Dodoma na mwendesha mashitaka wa serikali. Baada ya kufunguliwa shtaka hilo, Lissu ambaye alikuwa wakili wa Sugu aliitaka mahakama ifutilie mbali shtaka hilo kwani halina msingi wowote wa kisheria, na baada ya mabishano ya kisheria baina ya Lissu na wanasheria wa serikali kushindwa kuthibitisha kuwa neno Mpumbavu ni lugha ya matusi, hakimu ameamua kufuta shtaka hilo na ametangaza kuwa Sugu yuko huru na hana kesi ya kujibu.
Na Mjengwa

President Kikwete talks about U.S President Obama Visit to Tanzania

Tanzania High Commission in association with Urban Pulse Creative Media & Freddy Macha presents a short video interview of the Tanzanian President H.E Jakaya Kikwete talking about U.S President Barack Obama visit to Tanzania plus relationship between Tanzania and other developed countries e.g. China, German, US, Britain e.t.c.

MREMBO MWINGINE AMEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA YENYE THAMANI YA MILIONI 170.


Pretty saadah
SAADAH ALLY KILONGO
Siku ya graduu yake mwaka jana apooo
A BUSINESSWOMAN, Saada Kilongo (26), appeared before the Kisutu Resident Magistrate's Court in Dar es Salaam yesterday charged with trafficking narcotic drugs worth more than 170m/-.
Before Senior Resident Magistrate Nyigulila Mwasebo, the accused was not allowed to enter any plea to the charge. She was remanded until July 10, this year, when the case will be mentioned. 
Na  Juma Mtanda

Today's Quote

Today's Quote

Tamasha la Tigo Mini Kabaang Kufanyika Jijini Mwanza

Tigo Mini Kabaang
Tigo Mini Kabaang
Msanii wa bongo flava Diamond Platnumz akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya Jumapili pembeni yake meneja chapa ya TigoTanzania Bw. William Mpinga.
Tigo Mini Kabaang
Msanii Madee akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya jumapili pembeni yake meneja chapa ya TigoTanzania bw.William Mpinga na Diamond Platinumz.
Tigo Mini Kabaang Msanii Richie Mavoko akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya Jumapili kulia kwake ni Msanii Madee, meneja wa Tigo Bw. William Mpinga na Diamond Platniumz.

Msanii Bora wa mwaka Diamond Platinumz, Fid Q na wasanii wengine sita wanatarijiwa kupagawisha mashabiki zaidi ya elfu sitini katika tamasha la Tigo Mini Kabaang litakayofanyika jijini Mwanza (Rock city) Jumapili hii ya Juni 30.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo, Meneja wa Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga alisema kwamba lengo la tamasha hilo ni kujenga mahusiano ya karibu na wateja wao kwa kutumia sanaa ya muziki kama njia ya kutangaza huduma za Tigo na bidhaa zake za vifurushi kwa wateja wengi zaidi.

“Tunaamini kwamba tamasha hili litajenga mazingira mazuri yakufanya kampuni na wateja wetu kuelewana zaidi. Mwisho wa siku tunatarajia wateja wetu kujumuika nasi, kupata burudani yakutosha na kuelimishwa zaidi kuhusu huduma zetu mbali mbali zenye ubora na unafuu kama Mini Kabaang,” alisema Mpinga.

Mini Kabaang inatoa muda wa maongezi wa dakika 20 za bure, 50MB ya kifurushi cha intaneti, pamoja na ujumbe mfupi 100 kwa shilingi 475 tu kwa siku.

Mkutano huo wa waandishi wa habari pia ulihudhuriwa na wasanii wakubwa kama Madee wa Tip Top, Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Richi Mavoko, Recho, Kazi Kwanza, Diamond Platnumz na Fid Q, ambao ndio wasanii wa Bongo Fleva watakaopamba siku hiyo ya Jumapili katika viwanja vya CCM Kirumba kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 12 jioni.

“Mimi pamoja na wasanii wenzangu tunayo furaha kubwa kushiriki katika tamasha la Tigo Mini Kabaang litakalofanyika jijini Mwanza, hakika watu wa Rock city ni washabiki wakubwa wa muziki wetu, na tunatarajia kwenda kuwapa burudani ya kutosha,” alieleza Diamond Platnumz alipoulizwa kuhusu tamasha hilo.

“Binafsi nina furaha yakipekee kufanya tamasha langu la kwanza la wazi jijini Mwanza. Naamini hao mashabiki elfu sitini na zaidi wataonyesha mapenzi ya dhati kwa muziki wangu. Ninahamu sana ya kufika na kufanya tamasha hii,” aliongeza super staa huyo.

“Tamasha hili la Tigo Mwanza Mini Kabaang pia litawapa fursa mashabiki kujishindia zawadi mbali mbali kama vile simu, vocha, fulana za nembo ya Tigo na nyingine nyingi. Hakutakuwa na kiingilio siku hiyo, tunapenda kuwakaribisha kila mteja wa Tigo na mshabiki wa bongo fleva kujumuika na kushiriki nasi,” aliongezea Mpinga.

“MINI KABAANG” ni kifurushi cha siku ambacho mteja akijiunga anapata dakika 20 za muda wa maongezi ambazo anaweza kuzitumia kupiga simu kwenda mtandao wowote ule, pia anapata kifurushi cha 50MB ya intaneti na kuweza kutuma ujumbe mfupi 100 kwa mtandao wowote. Kutumia kifurushi hiki mteja anabidi apige namba *148*01#. Huduma hii inapatikana kwa wateja wote wa Tigo kwa gharama nafuu ya shilingi 475 tu kwa siku.

Tamasha za Mini Kabaang ni mfululizo wa maonyesho ya muziki yanayoandaliwa na Tigo, yamekwisha fanyika Morogoro, Moshi na sasa Mwanza. Mikoa mengine itakayofuata ni Mbeya, Dodoma na mikoa mingine.

MUONEKANO MPYA WA BANDARI YA ZANZIBAR kwa Picha Zaidi

 BANDARI YA ZANZIBAR
Hii ni hatua nzuri ya maendeleo kwa nchi nzima....ukiangalia kwa umakini picha hizi kwa ghafla unaweza usiamini kama ni zanzibar labda baadhi ya muonekano wa juu utagundua ndio kisiwani zanzibar...Maendeleo yaliyokuwepo kwenye bandari hii ni makubwa sana
ukilinganisha na Bandari ya zamaniilivyokuwa inaonekana lakini kwa sasa ni kitu kingine,ukifika bandarini hapo unaweza ukasahaukama upo kisiwani hapo...!Ni maendeleo makubwa kabisa kwa kisiwani zanzibar na ni
mfano wa kuigwa kokote pale kwahatua waliyopiga....Zifuatazo Ni Picha za muonekano huo mpya wa Bandari ya kisiwani zanzibar....!!
Inasemekana Mmiliki wa Azam Ndugu Bakhresa ndio aliedhamini
mchakato mzima wa kutengenezwa kwa bandari hiyo...!!
PONGEZI KUBWA KWA ZANZIBAR
 BANDARI YA ZANZIBAR
 BANDARI YA ZANZIBAR
 BANDARI YA ZANZIBAR
 BANDARI YA ZANZIBAR
Muonekano kwa usiku kwenye geti la kutokea bandarini hapo...!!
 BANDARI YA ZANZIBAR

 BANDARI YA ZANZIBAR
Sehemu ya ndani kwenye mapokezi....!!









 BANDARI YA ZANZIBAR