Pages

Sirudi Yanga Bila Mshahara Mil.5.6/- ;Kiiza

Yanga, Hamis Kiiza Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, Hamis Kiiza, amesema kwamba yuko tayari kukaa msimu mzima bila ya timu lakini hataweza kushusha kiwango cha mshahara wa mwezi cha Dola za Marekani 3,500 (Sh. milioni 5.6) ambazo anataka mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara wamlipe kuanzia msimu ujao.
Kiiza alikuwa analipwa mshahara wa Dola za Marekani 1,500 kwa mwezi katika misimu miwili aliyoichezea Yanga baada ya kusainiwa kwa kiasi cha Dola za Marekani 30,000 na sasa ameitaka klabu hiyo iliyoutema ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) impe fedha ya kusaini Dola za Marekani 45,000 (Sh. milioni 72) ili asaini mkataba mpya.
Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu kutoka kwao Kampala, Uganda, Kiiza alisema kuwa anaamini kiasi hicho cha fedha ndiyo kinalingana na thamani yake kwa sasa.
Mshambuliaji huyo ambaye yupo pia katika kikosi cha timu ya taifa ya Uganda (The Cranes) alisema kuwa mchezo wa soka ndiyo unaoendesha maisha yake na kwa kipindi hiki anatakiwa kufanya maamuzi sahihi ili aweze kujiandaa na maisha baada ya soka.
"Mimi kama nilivyowaambia sijabadilisha kitu, niko tayari hata kutorudi kama hawatakuwa tayari kunilipa, nami pia ninatoa mchango mkubwa kwa timu," alisema Mganda huyo.
Mbali na kiasi hicho cha mshahara ambacho kitakuwa ni cha juu ndani ya Yanga, Kiiza pia ameutaka uongozi umpatie nyumba ya kuishi na gari jipya la kutembelea akiwa hapa nchini.
Kiiza aliongeza kwamba licha ya kutofikia makubaliano na Yanga bado wakala wake hajampatia timu nyingine ya kwenda kufanya majaribio lakini wako kwenye mchakato huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Binkleb, aliliambia gazeti hili jana kwamba wao wako radhi kumuacha nyota huyo kama atashikilia msimamo wake huo.
Binkleb alisema kwamba wanaheshimu maamuzi yake kwa sababu wanajua ni kijana ambaye ana mipango na malengo yake kimaisha ambayo anataka kuyatimiza.
Kikosi cha Yanga kiko kwenye mapumziko na kinatarajia kuanza mazoezi upya Julai 2 mwaka huu kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi utakaofanyika kuanzia Agosti 24.
NIPASHE

PICHA za MAANDALIZI YA MAONYESHO YA SABA SABA 2013

 Saba Saba ya mwaka 2013
 Banda la Benki Ya NMB kama linavyoonekana katika Viwanja vya Sabasaba ambapo utaweza kupata Huduma Zote za kibenki ikiwemo na Kufungua Akaunti ya Chapchap na kupewa Kadi ya Kutolea Pesa kwenye Mashine za NMB Papo hapo kwa Gharama ya Tsh 10000 na huku ukiwa na Barua kutoka Ofisi ya Serikali ya Mtaa
 Saba Saba ya mwaka 2013
 Fundi akipaka rangi kwenye moja ya Banda la Wizara
Bunge la TanzaniaBunge la Tanzania liking'arishwa ili kuleta mvuto katika maonyesho ya Saba Saba ya mwaka 2013
 Saba Saba ya mwaka 2013
Fundi Mzigoni
 Saba Saba ya mwaka 2013
Bustani ikiwekwa safi kabisa
 Saba Saba ya mwaka 2013
Makabati yakiletwa tayari kwa maonyesho ya saba saba
 Saba Saba ya mwaka 2013
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar wakipita ndani ya viwanja vya sabasaba kwaajili ya Kutafuta vibarua vya hapa na pale
 Saba Saba ya mwaka 2013
 Saba Saba ya mwaka 2013
Kilimo Kwanza
 Saba Saba ya mwaka 2013
Magodoro yakipelekwa tayari kwa mauzo
 Saba Saba ya mwaka 2013
 Saba Saba ya mwaka 2013
Home Shopping Center watakuwa hapo
 Saba Saba ya mwaka 2013
Wakazi wa Jiji la Dar wakitafuta vibarua vyua hapa na pale
 Saba Saba ya mwaka 2013
JKT wazee wa kilimo na kujenga taifa

Maelezo ya Wakili Peter Kibatala Kumhusu Mteja Wake Henry Kilewo

Henry John Kileo alipigiwa simu na Maafisa wa Police Makao Makuu mnamo Tarehe 17/6/2013, wakimuarifu kwamba wanataka kufanya mahojiano naye.Hawakusema ni kuhusu nini.mara moja Kilewo akawasiliana nami kama wakili wa familia yao na Joyce Kiria ,nami nikawasiliana na maafisa hao kuwaarifu kwamba kwa kuwa nina majukumu kadhaa ya kkimahakama, na kwa kuwa Kilewo yuko nje ya mkoa, basi ninaahidi kama wakili kuhakikisha ninamepeleka binafsi Kilewo Makao Makuu Police mnamo Ijumaa ya tarehe 21/6/2013.

Tarehe 21/6/2013 tuliambatana mimi, Kilewo na John Mnyika (MB) mpaka Police Makao Makuu, ambapo Mnyika alituacha na Kilewo;mahojiano yakaanza.Kwa ujumla walimuhoji Kilewo mambo mbalimbali kuhusiana na tukio la kumwagiwa tindikali kijana aitwaye Mussa Tesha katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga mnamo mwaka 2011.Wakati mahijiano hayo yanafanyika,tayari kulikuwa na Case ya jinai ikiendelea huko Igunga, ambapo washtakiwa Wanne (4) ambao ni makada wa Chadema kutoka maeneo mbalimbali nchini walishtakiwa kama mshtakiwa nambari moja mpaka nne.Walishtakiwa kuhusiana na tukio hilo nililolisema, la Mussa Tesha kumwagiwa Tindikali.Walishtakiwa chini ya vifungu vya sheria ya kanuni ya adhabu, (Penal Code, na si ugaidi).

Baada ya mahojiano na Police yaliyomalizika kwa Kileo kuandikisha statement mpaka mnamo saa 11.30 hivi
za jioni ya hiyo Tarehe 21/6/2013, Police walimnyima Kilewo dhamana, na wakampeleka remand iliyoko Central Police Station,akalala huko.

Jumamosi ya mnamo tarehe 22/6/2013, mimi wakili, Joyce Kiria na John Mnyika tulifika Central Police station, ambapo OCS wa hiyo Central Police Station alituarifu kwamba amri alizonazo ni kwamba Kilewo haruhusiwi kuonana na mtu yeyote. Kama wakili nilijadiliana masuala ya kisheria na OCS, ikalazimu kuwasiliana na maafisa wa Police Makao Makuu ambao hatimaye waliniruhusu mimi kama wakili kwa mujibu wa sheria kuonana na mteja wangu.

Tukazungumza na kupeana "moyo", nikahakikisha amekula chakula kilicoletwa na mkewe Joyce Kiria (ambaye muda wote alikuwa akimuangalia mumewe kwa mbali tu,kwani mazungumzo yangu na Kilewo yalifanyika faragha).

Mnamo saa 7.30 hivi tuliondoka sote (wakili, Kiria na Mnyika), na kukubaliana kurudi tena Central Police Station Jumapili ya Tarehe 23/6/2013 kumtembelea tena Kilewo, na pia kufahamu mipango hasa ya jeshi la Police kuhusu Kilewo kwani mpaka tunaondoka si wakili wala mkewe Kilewo aliyefahamishwa rasmi kuhusu mipango hiyo.

Nikiwa Nyumbani nilipokea simu toka kwa Joyce Kiria akiniarifu kwamba amefika Central Police Station jioni ya Jumamosi ya tarehe 22/6/2013 na kuarifiwa tu kwa mkato kwamba Henry John Kilewo "ameondoka".

Ukweli kama mke alikuwa amechanganyikiwa, na jukumu la kwanza lilikuwa kumtuliza kisaikoilojia kwani nilifahamu kina Kilewo walikuwa wamepata mtoto muda si mrefu huko nyuma;kwa hiyo hali ya Joyce ilikuwa delicate sana kiafya na kisaikolojia.

Nikapambana kama wakili kwa kutumia uzoefu na contacts (P.R) ili kupata tarifa ya aliko mteja wangu.
Niliariwa tu "off record" na maafisa wa Police kwamba Kilewo amesafrishwa kwa ndege ya Precision kuelekea Tabora kupitia Mwanza chini ya ulinzi wa maafisa Senior wa Police ili kule Tabora afunguliwe Case. Sikuwa na mawasiliano yeyote na mteja wangu, na hizo taarifa "off record" ndo cha pekee tulichokuwa nacho mimi, Joyce Kiria na uongozi wa Chadema kuhusu nini kimemsibu Henry Kileo.

Niliendelea kupambana kupata taarifa rasmi, na hatimaye Jumapili ya Tarehe 23/6/2013 majira ya saa 6 hivi (noon) ndipo nilipopigiwa simu na mmoja wa maafisa waliomsindikiza Kilewo kuelekea huko Tabora kwa utaratibu ule ule wa "off record", na kuniunganisha na Kilewo, ambapo nilizungumza naye kwa kifupi kumjulia hali na kumuhakikishia kwamba tutapigana kwa uwakili wetu wote kwa ajili yake.

Kwa hiyo mpaka muda huo hatukuwa bado na uhakika wa 100% kwamba Kilewo yuko wapi hasa. Kw wale mawakili wenzangu wanafahamu kwamba huwezi tegemea taarifa za kusikilizishwa mteja kwenye simu ambayo hata si ya kwake.Wala huo si ushahidi wa alipo mtu huyo kisheria.

Lakini ikatubidi ku-"assume" kwamba Kilewo yuko/atapelekwa Tabora kushtakiwa.mimi na Prof Abdallah Safari tukaanza maandalizi ya upesi upesi ya safari kuelekea Tabora kwa gari (kwani ndege kuulekea Tabora ni Jumamosi na Jumatatu tu). Tuliondoka kwa gari ya makao makuu ya Chadema Jumapili ya tarehe 23/6/2013, majira ya saa 11.30 hivi za jioni. Tulisafiri usiku kucha, na tulichukuwa "risk" ambazo kwa kawaida tusingechukuwa, ikiwemo kupita katika mapori maarufu kwa utakaji;kilichotusukuma na kutupa moyo ni kwamba Henry John Kilewo yuko mahali ambapo anatuhitaji sana, na hana tumaini lingine bali sisi mawakili wake.

Tukisafiri usuku kucha na kufika Tabora asubuhi ya Jumatatu tarehe 24/6/2013, majira ya saa 2.30 asubuhi;tumechoka hakuna mfano.Tukabadili mavazi upesi upesi na kuvaa suits zetu na kukimbilia mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora, ambapo turiarifiwa kuwa wao hawana taarifa zozote za Kilewo. Tukaelekea Makao Makua ya Police Tabora;jibe likawa ni lile.

Maana yake ni kwamba sisi mawakili wa Kilewo, tuko Tabora ambayo ni kubwa has, na hatujui mteja yuko wapi hasa. Nikafanya juhudi zile zile za "off record", na kufahamishwa kwamba Kilewo alishikiliwa Police Station ya Nzega (masaa matatu toka Tabora), na kwamba yuko njiani kuletwa Tabora. Hatukuwa na uhakika bado, ila ilitulazimu kushikilia hako kataarifa kasiko rasmi, na kuendelea na maandalizi ya case.

Majira ya saa 9 hivi za alasiri ya Tarehe 23/6/2013 Kilewo, akiwa chini ya ulinzi mkali sana wa FFU katika Land Cruisers Mbili za Police waliwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora; hajala tangu jana yake.
Alikuwa yeye na wenzake wanne ambao walikuwa wamefutiwa mashtaka kwa hati ya "Nolle Prosequi" huko Igunga, kisha kukamatwa tena mara moja na kusafirishwa kwa ulinzi mkali sana mpaka Tabora.

Ukweli ni kwamba tulivyoonana na Kilewo si mawakili wala KIlewo mwenyewe aliyejizuia kulengwa na machozi;yeye akimshukuru MUNGU kwamba tumepambana na yote mpaka Tabaora kwa ajili yake kwa kasi vile, nasi kwamba hatimaye tumeonana na mteja wetu.
Tukaingia Mahakamani, Kilewo na wenzake wakasomewa mashtaka mawili; moja chini ya sheria ya kuzuia ugaidi kwamba walimteka kwa nia ya ugaidi Mussa Tesha huko Igunga, Tabora na la pili kwamba walimdhuru kwa kumwagia Tindikali.

Makosa ya Ugaidi hayana dhamana.
Mawakili tulipambana na kutoa hoja za kisheria nne (4) dhidi ya uhalali wa mashtaka yenyewe na utaratibu wa kufungua case husika. Tumeoimba mahakama kufuta mashtaka ya ugaidi, au la iamuru kila mshtakiwa arudishwe kushtakiwa mahali alikokamatwa (mfano Kilewo, Dar es Salaam).

Uamuzi wa Mahakama ni tarehe 8/7/2013.
Kabla ya kuondoka Tabora jana, tulipita kumuaga Henry Kilewo na wenzake katika gereza la Uyui. Wote wako na combat zao za chama chao, na wako imara, hasa baada ya kuona mawakili wako imara.

Cha msingi ni kuomba MUNGU aipe mahakama ujasiri.
Peter Kibatala, Advocate.
Wavuti.

Comparison of the NBA’s big 3: Michael Jordan, Kobe Bryant, LeBron James

Michael Jordan, Kobe Bryant, LeBron James

Barack Obama Arrives in Senegal, The Start of Africa Tour

US President Barack Obama opened a week-long trip to Africa on Wednesday by touching down in the Senegalese capital of Dakar. The three-country visit is aimed at overcoming disappointment on the continent over the first black US president's lack of personal engagement during his first term.

STUDY IN INDIA. ADMISSION OPEN FOR ACADEMIC YEAR 2013-14 AT JAIN UNIVERSITY

JAIN UNIVERSITY

Feast - Magna Carta Holy Grail - Jay-Z - Leak - Timbaland

Nelly - Dilemma ft. Kelly Rowland (Video) Replay

MAPOKEZI YA MFALME MSWATI TANZANIA

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Mfalme Mswati wa (ii) wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo Juni 26, 2013. Mfalme Mswati wa ii, ametua nchini kwa ajili ya
kuhudhuria Mkutano wa 'Smat Patnership' unaotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu.
Mfalme Mswati ii,
Picha juu na chini ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mfalme Mswati ii, baada ya
kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Juni 26, 2013. Mfalme Mswati wa ii, ametua nchini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 'Smat Patnership' unaotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu.
Mfalme Mswati ii,
Mohammed Gharib Bilal,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Mfalme Mswati ii, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Juni 28, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 'Smat Patnership', unaotarajia kuanza Juni 28. Kushoto ni mke wa Mfalme Mswati.
Picha na OMR

Walinzi wa Obama Watia Fora, Mawasliano Yatazima Air Port Anytime..!!?!

Walinzi wa Obama
Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere, Moses Malaki alisema jana kwamba ratiba za uwanjani
hapo zitabadilika kutokana na uzito wa ugeni huo.
Alisema kwa kawaida anapokuja kiongozi mkubwa wa
kitaifa katika uwanja huo hakuna ndege inayoruhusiwa kutua kwa kipindi cha nusu saa.
“Ni kweli hali hiyo pia itakuwapo
atakapokuja Rais Obama na safari
za ndege zitabadilika kulingana na ratiba ya kutua na kuondoka kwa
Rais huyo,” alisema Malaki.
Pia alisema ulinzi katika uwanja huo umeimarishwa
kwa mwezi mmoja sasa na tangu wakati huo,
maofisa wa usalama wa Marekani wamekuwa wakifika kwa nyakati mbalimbali.

“Sijawahi kuona ulinzi mkali kama huu, wamekuja
marais wengi hapa nchini lakini ulinzi huu ni wa kutisha, sijui
kwa sababu gani?” alisema Malaki.
Alisema awali, wakati maofisa hao walipoanza
kuwasili nchini hawakutambua ni mgeni
gani anayetarajia kufika lakini baadaye walipelekewa taarifa kuwa ni Rais
Obama na baadaye walitaarifiwa kuwa angetua saa 8.40 mchana, Julai Mosi.
Mkurugenzi huyo alisema Rais Obama atakuja
na ndege nne, moja itakayombeba,
ya pili kwa ajili ya mizigo, ya tatu itakuwa ya waandishi
wa habari na maofisa wa usalama na ya mwisho ni kwa ajili ya dharura ambayo itaegeshwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)
Malaki alisema maofisa wa Marekani wanaowasili nchini wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali za kuhakikisha kuwa hali ya usalama
inaimarishwa na kuwaacha wazawa wakifanya shughuli za kawaida.
“Ulinzi ni mkali mno, yapo masharti kadhaa
wanayoyataja kuwa yatatumika
kwa watu watakaoingia
eneo la uwanja au kuisogelea ndege ya Rais Obama. Jamaa
wameweka masharti magumu,” alisema.