Hivi ndivyo hali ilivyo katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Arusha Tanzania
MBUNGE wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi amenusurika kufa wakati akielekea Jijini Arusha kuwahi kuaga miili ya marehemu waliouawa kwa mabomu yaliyolipuliwa siku chache zilizopita kwenye mkutano wa Chadema jijini hapa.
Joseph Mbilinyi aliamua kwenda kuungana na Wananchi wa Arusha na wanachama wa Chadema, amepata ajali hiyo maeneo ya Kateshi Wilaya ya Hanang.
Ajali hiyo imetokea baada ya gari la Mbunge huyo kugongana na gari la abiria lililokuwa katika mwendo kasi,na katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa zaidi ya gari la mbunge huyo kuharibika vibaya.
Mbali na Gari Sugu kuahribika vibaya taarifa kutoka Arusha pia inaeleza kwamba Gari la Tundu Lissu pia limepigwa bomu kama ilivyokuwa gari la Lema.jijini Arusha hali bado si shwari kwani Askari Polisi wanaendelea kutawanya waandamanaji walioamua kuingia mitaani huku wakiwa na mji kwenye madumu kwa ajili ya kuwa kila wanapopigwa mabomu na Polisi
Lema anusurika kufa, akimbilia kwa wachoma kiti moto!

WAKATI hali ikizidi kuwa mbaya jijini Arusha kufuatia mapambano ya raia na Jeshi la Polisi,Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amelazimika kukimbilia kwa wachoma nyama ya Nguruwe, (kiti moto).
Lema ambaye alinusurika kupigwa na bomu lilorushwa na Askari wa Jeshi la Polisi na kuharibu gari lake alikuwa akijaribu kuwatuliza wananchi walioanza kukusanyika katika vikundu, wakijadii amri ya Serikali ya kukataza miili ya watu waliofariki Dunia katika shambulio la kigaidi isiagwe katika viwanja hivyo.
Kabla ya Lema kupigwa mabomu na kukimbilia kwa wachoma nyama ya nguruwe hao alikuwa akisema, "jaribuni kuvumilia tunajaribu kuwasiliana Serikali ya Mkoa, ili watupe kibali ya kuleta miili ya wapendwa wetu hapa,kuweni wastaarabu kwa sababu mbele yetu kuna wanausalama ambao wanalinda amani,ingawa kufa ni kufa tu, wenzetu wamesha kufa na sisi ipo siku tutakufa, lakini kila anayetangulia lazima tumzike kwa heshma zote"alisema Lema kabla ya kupigwa bomu na Polisi.
Kauli hiyo ilizidi kiwachefua Polisi ambao walishatangaza amri ya watu kutawanyika katika viwanja hivyo, kwa ajili kuweka hali ya usalama wa eneo hilo ambapo walisema kwamba hakutakuwa na suala la kuaga maiili ya watu hao katika eneo hilo.
Mwandishi wa Habarimpya.com pia alikimbilia kwa wachoma kito moto kwa nia ya kujificha kufuatia mabomu kurushwa kila kona ndipo alipokutana na Mbunge huyo,hata hivyo alipojaribu kuzungumza naye alikataa kujibu lolote huku akiwa ameinamisha kichwa chini,kabla ya kuchukuliwa na gari ndogo aina Toyota Corola na kutokea kusiko julikana.
Habarimpya.