Pages

Wanajeshi Wanne Wamefariki Wakielekea Mtwara Kutuliza Ghasia

41KJ Wanajeshi wakipokea mwili ya askari mwenzao. Picha hii haihusiani na habari hapo chini
WANAJESHI wanne wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) waliokuwa wakielekea Mtwara kusaidia kutuliza ghasia zinazoendelea mjini humo wamefariki dunia, huku wengine 20 wakijeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali wilayani Nachingwea mkoani Lindi.
Habari zilizopatikana hivi punde na kuthibitishwa na baadhi ya mashuhuda zinasema kuwa ajali hiyo ilihusisha lori la wanajeshi hao na gari nyingine imetokea eneo la Kilimani Hewa, kilomita mbili toka kambi ya Jeshi hilo ya 41KJ wilayani humo.
Taarifa hizo zinasema kuwa jumla ya wanajeshi 31 walikuwa kwenye msafara huo na kwamba 20 wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitali ya wilaya hiyo, huku wengine saba wakitoka salama bila ya kuwa na majeruhi yoyote.
Inaelezwa kuwa mwendo kasi na kona kali iliyopo eneo la tukio ndiyo chanzo cha ajali hiyo, ingawa Polisi bado haijathibitisha taarifa hizo kuhusiana na vifo vya wanajeshi hao wanne walioelezwa wamefariki katika ajali hiyo. Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Viginia Ole Swai, amenukuliwa na kituo cha Radio One Stereo akisema huenda vumbi nalo lilichangia kutokea kwa ajali hiyo baada ya gari hizo kugongana katika ajali hiyo ambayo imepoteza uhai wa wapiganaji hao wa JWTZ wanne na wengine kujeruhiwa ambapo wapo hospitali wakitibiwa.

Nakupenda Tanzania

Nakupenda Tanzania

Obama Skips Kenya; A Frustrated Kenyan Responds..! (Video)

President Barack Obama will leave on a first African tour next month, visiting Senegal, Tanzania and South Africa, but his itinerary released on Monday bypasses Kenya, an ancestral homeland.

NAKUJA KWENU NA “MSULI TEMBO MATOKEO SUNGURA” NIKKI MBISHI

Nikki Mbishi
Nikki Mbishi soon, kuachia wimbo ambao hautakuwepo kwenye media yoyote ile bali kwenye simu na computer za mashabiki wake.Nikki kupitia ukurasa wake wa facebook amesema, mtu kuipata single hiyo inabidi achangie shilingi 1000, na atapokea oda kupitia comments za ukurasa wake ambapo zoezi hilo anategemea kulianza siku ya jumatatu.
Wimbo huo ambao amaupa jina la “Msuli Tembo Matokea Sungura” unalenga kuwapa moyo watu wote wanaotumia nguvu, akili na jitihada kwa kiasi kikubwa lakini wanachokipata ni kidogo kulinganisha na walichokiwekeza
Nikki Mbishi BabaMalcom
Kuna track yangu mpya mahususi kwa mashabiki tu wala sitaitoa kwenye media inaitwa “MSULI TEMBO MATOKEO SUNGURA” ikilenga kuwapa moyo watu wote wanaotumia nguvu,akili na jitihada kwa kiasi kikubwa lakini wanachokipata ni kidogo kulinganisha na walichowekeza,k ama wewe ni mmoja wa watakao niunga mkono kwa kuchangia Tsh 1000 ili uipate unaweza kupost comment yako na zoezi litaanza Jumatatu!#Asanteni.

RAW FOOTAGE: THREE DEAD BODIES LYING ON THE STREET OF WOOLWICH LONDON!

May 22st, 2013 -PERSON DEAD WITHOUT A HEAD CONFIRMED FOR BRITISH SOLIDER. TWO SOMALIANS CRITICALLY INJURED.
One man is reported dead and two others injured amid reports of a shooting incident close to the Royal Artillery Barracks in Woolwich this afternoon.One witness reported seeing a man beheaded in the street in an attack by two men.
The report also said that police officers opened fire after the attack in John Wilson Street in Woolwich.
There were reports that shots were fired after an apparent sword attack near the army base.
Pictures posted on Twitter appear to show two men lying on the road in Woolwich.
David Dixon, the head of Mulgrave Primary School, told the BBC that he walked out of the school gates and saw a body lying in the street. "We shut all the gates and made sure all the children were inside," he said.
Mr Dixon also confirmed hearing gunshots.
The Metropolitan police would only say officers had been called to reports of 'an assault' on John Wilson Street.
Wellington Street has been sealed off and an air ambulance has arrived on the scene.

USIKU WA HIP HOP, THE VODACOM MIC KING..! KURINDIMA J’MOSI HII DAR LIVE

Wakali tisa wa Hip Hop wanaowania gari aina ya Toyota FunCargo (new model), katika pozi mbele ya gari lao. ILIPANGWA, ikapangika. Baada ya kusubiririwa kwa muda mrefu, hatimaye msimu mpya wa shoo ya Usiku wa Hip Hop (2013) unachukuwa nafasi Jumamosi hii ndani ya Ukumbi wa Dar live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar.
Toyota FunCargoWasanii wanaotamba kwenye gemu la Hip Hop, Kala Jeremiah, Fid Q, Nay wa Mitego, Joh Makini, Stamina na wengine kibao pamoja na washiriki wa Shindano la The Vodacom Mic King watakamua shoo baab’kubwa kuweka historia mpya ya burudani.
Meneja Matukio wa Ukumbi wa Dar Live, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ amewahakikishia mashabiki wote wa muziki wa Hip Hop kuwa Jumamosi kutasheheni matukio kibao, ulinzi mzito utakuwepo pamoja na parking kubwa ya magari hivyo watu wafike kwa wingi watainjoi kwa nafasi na kuondoka salama ukumbini.
“Vijana tisa waliosalia katika Shindano la The Vodacom Mic King watapanda jukwaani na kushusha mistari ambapo mshiriki mmoja anatarajiwa kuondoka na gari jipya aina ya Toyota FunCargo (new model),” alisema Abby Cool na kuongeza:
“Mashabiki wanaweza kulifuatilia shindano hilo kupitia Runinga ya DTV kuweza kujua jinsi ya kuwapigia kura.”
The Vodacom Mic King
Washiriki hao na namba zao za ushiriki kwenye mabano ni Ally (MK 02), Anold (MK 03), Bahati (MK 05), Boniface (MK 07), Emmanuel (MK 10), Ibrahim (MK 12), Karrys (MK 13), Lusajo (MK 14) na Martin (MK15). Jinsi ya kuwapigia kura, wasomaji wanatakiwa kuandika neno MK wakiambatanisha na namba ya mshiriki kisha kutuma ujumbe huo kwenda namba 15564.

OFA ZAIDI KWA MSHINDI
Mbali na mshindi kuondoka na gari, Mrisho aliongeza kuwa washindi watatu wa nafasi za juu watajipatia dili la kurekodi singo mojamoja kutoka kwa prodyuza kiwango aliyezalisha ngoma kali Bongo ikiwemo ya Kundi la Kigoma All Stars iitwayo Leka Dutigite, Tudd Thomas.

TUZO KUTOLEWA
Mrisho alitiririka na mistari kuwa, mbali na shoo kali kutoka kwa wakali hao wa Hip Hop, kutakuwa na kipengele cha kutoa tuzo za muziki wa Hip Hop katika vipengele tofauti hivyo mashabiki pia...

MAONI YA CARTHBERT KAJUNA KUHUSU TAALUMA YA UANDISHI WA HABARI NDANI YA MAGAZETI TANDO/MITANDAO YA KIJAMII

Kajunason  
Watu wengi kwa sasa wameibuka na kutokea kuipenda fani ya uandishi wa habari bila kujua misingi na miiko ya uandishi wa habari. Tatizo moja ambalo limeonekana ni kubwa sana ni utandawazi ambao umekuwepo na kutokea ibuko la kila kijana kufungua gazeti tando (blog).

Hatukatai kuja kwa magazeti tando ila naomba tujiulize, yanatumika ipasavyo ama ndiyo limekuwa ni wimbi vamizi lenye kutoa ama kusambaza habari hata zile zisizokuwa na vyanzo kamili na visivyojitosheleza.Kwa sasa imezuka tabia ya wanaojiita wamiliki wa magazeti tando,wengi wao kukopi na kupaste vitu wanavyoviokota katika mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter, facebook na mingine mingi.
Sina nia ya kumsema mtu bali napenda tuelimishane kama vijana wenzangu,ambao wametokea kuipenda fani ya uandishi wa habari, wakumbuke kuwa fani ya uandishi wa habari ina miiko na maadili yake, mfano. Katika kuandika habari za mazingira, siasa, elimu, uchumi, michezo, burudani ukiangalia habari hizi zote zina misingi na miiko yake.

Leo hauwezi kumchukua mwandishi wa habari za michezo ukamwambia aandike habari za uchumi kwa vile hatakuwa na takwimu za uchumi na hata akiandika hiyo habari na ukiisoma utakuwa unajiuliza maswali mengi bila kupata majibu.
Vile vile ni vizuri vijana wenzangu kutambua kuwa kila kazi ina mipaka na misingi yake, juzi juzi nilisoma habari katika gazeti tando moja wapo ikisema, ‘ALIYEONGOZA MAANDAMANO YA IRINGA MHESHIMIWA MCHUNGAJI MSIGWA ASWEKWA NDANI’ nilijiuliza maswali mengi ambayo kiukweli nilikosa majibu yake, kuona huyu aliyeandika hiki kichwa cha...

Abby Skills ft Chege - Shani na Jenny (Audio)

Abby Skills ft Chege - Shani na Jenny

WANAOVAA VIMINI KWENYE FILAMU WANAJIUZA: MWAKIFWAMBA

Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon MwakifwambaRAIS wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifwamba amesema wasanii wanaovaa mavazi yasiyo na staha ikiwemo vimini kwenye sinema wanajiuza.
Mwakifwamba aliyasema hayo katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, akiwa ameongozana na msanii Riyama Ally.
Kauli hiyo ya Mwakifwamba imekuja siku chache baada ya sakata la uvaaji vimini na udhalilishaji wanawake na wototo kwenye filamu kuzungumziwa bungeni, Dodoma.
APIGIA MSUMARI
“Hili suala nimeshalikemea kwa muda mrefu sana... naamini kama ni watu wa kuelewa watakuwa wameelewa na wale ambao wanaendelea na hayo mambo maana yake ujue wana mambo yao.
“Siyo wote wanaoingia kwenye filamu ni wasanii wa kweli, wengine wanatumia tasnia hii kutafuta mabwana ndiyo maana wanavaa mavazi ya ajabu ili waonekane, jambo ambalo tunalikemea kila wakati.
“Sikatai wakati mwingine kuna ‘scene’ zitahitaji uhusika fulani kama uchangudoa lakini utakuta msanii anatakiwa kuvaa uhusika wa ofisini, yeye anavaa vinguo vya hovyo, maana yake ni nini kama si kutafuta soko?” alisema Mwakifwamba na kuongeza:
“Imefika wakati wasanii wanatakiwa wabadilike kwani hali ilipofikia siyo pazuri. Bado msanii anaweza kuonekana ana kiwango kizuri bila kuvaa nguo zinazomdhalilisha na kumtafsiri vibaya mbele ya jamii.”
Akasema: “Sasa nasema hivi, yeyote atakayekiuka utaratibu tuliokubaliana tutamchukulia hatua. Hatutamfumbia macho. Tunahitaji kuwa na tasnia yenye heshima.”
RIYAMA SASA
Mkali wa kucheza na hisia, Riyama naye alitoa maoni yake kuhusu mavazi na mwenendo mzima wa filamu za Kibongo ambapo kwa upande wake alisema anaamini wanaofanya hivyo wanatafuta kuwa mastaa kwa njia ya mkato.
“Tatizo ni ulimbukeni wa kuiga wasanii wa nje. Wasanii tunakiwa kujitambua na kufahamu na kulinda utamaduni wetu. Wasanii wengi hawajui thamani zao, jamani ustaa siyo kukaa uchi.
“Tujue kuwa kwenye filamu siyo sehemu ya kutafutia mabwana. Kuonesha urembo wetu wa nje na wa ndani kwenye hadhara siyo kitu kizuri kwa utamaduni wetu... hao wanaofanya hivyo wanasababisha wasanii wote tuonekane machangudoa,” alisema Riyama.
GPL

Clyde Carson - Slow Down ft. The Team (Video)