-Wadaiwa kulitumia kuomba rushwa kwa mfanyabiashara
-Washikiliwa kituo cha polisi kwa mahojiano
JESHI la Polisi mkoani Morogoro limeingia kwenye kashfa nzito baada ya askari wake watatu na raia wanne kukamatwa wakiwa na kichwa cha binadamu. Tukio hilo lilitokea Mei 7 mwaka huu katika eneo la Mgudeni- Dumila wilayani Kilosa. Inaelezwa kuwa polisi hao kwa kushirikiana na raia hao walikwenda nyumbani kwa mfanyabiashara Samson Mura na kutaka kumbambikizia kesi ya mauaji.-Washikiliwa kituo cha polisi kwa mahojiano
Mbali ya kubambikizia kesi hiyo, polisi hao wanadaiwa kuomba wapewe Sh milioni 25 na mfanyabiashara huyo ili wasimpeleke kituoni. Wakizungumza na MTANZANIA jana, baadhi ya wananchi walisema wameshangazwa na askari hao ambao wawili ni wa Kituo cha Polisi Dumila na mmoja wa Kituo cha Polisi Mvomero.
Walisema siku ya tukio, polisi hao walifuatana na raia mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kwa ajili ya masuala ya usalama.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mgudeni,Zaituni Kifutu alisema walishangazwa na tukio hilo. “Tumeshangazwa mno na askari hawa… sijui walichukulia wapi mafunzo yao? Kama walibaini kuwapo tukio hili kwa nini hawakutaka kulifikisha kituoni? “Inasikitisha mno, eti wao kwa kushirikiana na mfanyabiashara wanakwenda kudai kwa mwanakijiji mwenzetu wapewe Sh milioni 25… haiingi akilini hata kidogo wakamate mhalifu halafu washirikiane kwenda kuomba fedha.
“Tunaona na mazingira ambayo askari na raia huyo ambao walifika kwenye nyumba ya..