Wakamatwa kwa Kujihusisha na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu
Kaimu Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Tatu Burhan Jumla ya watu 12, 864, wakiwemo Watanzania na raia wa nje, wamekamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola kwa kosa la kujihusisha na biashara haramu ya kusafirisha binadamu.Akizungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Tatu Burhan, alisema kukamatwa kwa watu hao kumetokana na kuimarishwa kwa mfumo wa usimamizi wa mipaka na udhibiti.
Alisema raia wa nje wanaofanyabiashara hiyo wanashirikiana na wenyeji, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa nchi, hivyo ni vyema wakaacha tabia hiyo kwa kuweka uzalendo mbele.
Aidha, aliiomba serikali kuongeza vifaa vya kisasa kutokana na kuwepo kwa mbinu mpya na matumizi ya silaha na kuingizwa kwa silaha za kivita ambazo hutumika kuleta madhara kwa jamii.
Idara hiyo nchi nzima ina askari wasiozidi 3,000 huku mahitaji yakiwa ni 8,000, ambapo mpaka wa Tanzania ukiwa mkubwa unaopakana na nchi nyingi na..
Waganga Wajitokeza Kupambana na Jini Mahaba Linalo Mtesa Lady J'dee
WAGANGA wanaodai kuwa ni wataalam na wana uzoefu wa kupambana na jini mahaba linalomsumbua Mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, wamejitokeza huku kila mmoja akiomba apewe nafasi ya kumtibu bure.
Mmoja wa wataalam hao aliyejitambulisha kwa jina la Jumaa wa Magomeni, Dar alisema: “Nimesoma habari kuhusu Jide, mimi naweza kumtibu tena bure, mpe namba yangu na mwambie anipigie.”
Mwingine ambaye hakupenda jina lake liandikwe alisema: “Nimesikitika sana kusoma hii habari ya huyu msanii Lady Jaydee, kwa kifupi naweza kumtibia free of charge.”
Kufuatia maombi ya wataalam hao, mwandishi wetu alijitahidi kumtafuta Jide bila mafanikio lakini juzikati kupitia kipindi chake cha Diary ya Lady Jaydee alionekana akipewa matibabu na ustaadhi mmoja, mazingira yanayoashiria kuwa huenda mambo yametulia.
CREDIT : GPL

Askari Aliyemwua kwa Risasi Mwalimu NMB Afukuzwa Kazi, Njombe
JESHI la Polisi mkoani Njombe, limemfukuza kazi askari wake PC Gelvas Joseph, mwenye namba 9790, kwa kosa la kufanya mauaji ya mwalimu wa Shule ya Sekondari Kitulo, wilayani Makete.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Focus Malengo, alisema askari huyo alifanya kosa hilo Februari 27 mwaka huu kwa kumpiga risasi kifuani mwalimu Castory Sote (31), na kusababisha kifo chake papo hapo.
Alisema askari huyo amefukuzwa kazi baada ya uchunguzi wa tukio hilo kukamilika na kubaini alikiuka kanuni za utumishi ambapo hivi sasa anakabiliwa na mashtaka.
Aliongeza kuwa, kosa hilo alilifanya akiwa lindoni kwenye Benki ya NMB, tawi la Makete, ambapo marehemu alikuwa akichukua fedha katika mashine za benki hiyo.
Ilidaiwa kuwa, siku ya tukio hilo kulitokea malumbano kati ya mwalimu huyo na askari ambaye alimtuhumu marehemu kuendesha pikipiki bila kuvaa kofia ngumu (helmet) kichwani. Hali hiyo ilizua mzozo kati yao baada ya marehemu kudai kuwa, polisi huyo si askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani.
Imeandikwa na Mercy James, Njombe (via Majira)

CAR FOR SALE

DETAILS
Year: 2003 (Imported this January, 2013), Mileage: Almost 52,000 km, Displacement (CC) 1,790 with VVT-i Engine, Body Type: Station Wagon, Color: Metallic Grey, Fuel: Gasoil/ Petrol, Gear box type: Automatic, Sitting capacity: 7, Motor vehicle license and Insurance validity: Expires January 2014, Other details: All duties paid, Good tires, New Break Pads, No mechanical problems, Serviced upon arrival, In very good shape and condition: Reason for Sale: Bought for a wife who wants 4x4. Needs 15 milion. (Tshilngs)

Click read more for more pictures..
Blog Zote za Bongo, kwa Mablogger,Wasomaji na Wadau!!
Kama Unasumbuka kukumbuka majina ya blog uzipendazo hii itaksaidia!!
Blog zote ndani ya Blog 1.
Inapatikana Hapa >> http://bongoblogs.blogspot.com
Mwambie Rafiki Amwambie Rafiki..!!

Video ya Kukamatwa kwa Lwakatare CHADEMA Yafafanua, CCM na Usalama wa Taifa Wahusika Wakuu
'' Tunamjua anayeendesha mbinu za kutuchafua-Dk Slaa.
polisi wapekua nyumba yake kwa mara ya pili, aendelea kushikiliwa na jeshi hilo.

Polisi wambana Lwakatare. -Dk. Slaa: Video ya Lwakatare ni Feki
Lwakatare alikamatwa juzi makao makuu ya chama hicho na kupelekwa katika Makao Makuu ya Polisi kwa mahojiano.
Polisi wamezidi kumbana Mkuu wa Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare baada ya kupekua nyumbani kwake kwa siku ya pili mfululizo.
Lwakatare, ambaye ni mbunge wa zamani wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia CUF, alikamatwa juzi mchana kwa kutuhumiwa kwa kufanya uchochezi wa uvunjifu wa amani baada ya kunaswa kwenye picha ya video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii
Upekuzi wa pili
Nyaronyo Kicheere, ambaye ni Mwanasheria wa Lwakatare, aliliambia gazeti hili jana kuwa mteja wake, ambaye anashikiliwa na polisi hao, alipelekwa nyumbani kwake Kimara-King’ong’o jijini Dar es Salaam kwa ajili ya upekuzi huo.
Ilikuwa mara ya pili kwa Lwakatare kupekuliwa kwani mara ya kwanza ilikuwa juzi jioni baada ya kuhojiwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi. Lwakatare, ambaye alitolewa Kituo cha Kati cha Polisi, alipelekwa jana kwa msafara wa magari mawili ya polisi chini ya ulinzi mkali.
Nyaronyo alisema kuwa msafara huo uliondoka saa 10.00 jioni kwa ajili ya safari hiyo ya Kimara wakitokea katikati ya Jiji la Dar es Salaam kilipo Kituo cha Kati cha Polisi. Alisema kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya...

Subscribe to:
Posts (Atom)