ALAZIMIKA KUJIFICHA NYUMBANI KWA WATU
PADRI wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza, Alfonce Twimann’ye mwishoni mwa wiki alilazimika kujificha katika nyumba ya watu baada ya kukimbizwa na watu wasiojulikana eneo la Nyakato mkoani Mwanza.
Habari za kuaminika na zilizothibitishwa na padri huyo maaarufu kwa mahubiri mkoani hapa, zimesema kuwa watu wawili waliokuwa katika pikipiki, walimwandama wakati akielekea Kitongoji cha Mahina kutoa huduma za kiroho kwa mmoja wa waamini wa Kanisa Katoliki.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumamosi kwa njia ya simu, Padri Alfonce alisema akiwa katika kituo kimoja cha mafuta eneo la Nyakato wiki iliyopita, alishangaa kuona kwa mbali kikundi cha watu kikimtazama na baadhi yao wakioneshana vidole kumwelekea alipokuwa ameegesha gari.
Padri huyo aliongeza kuwa, wakati anaondoka baada ya kuweka mafuta katika gari, watu wawili waliokuwa katika pikipiki walimfuata, kwa mwendo wa kasi jambo lililompa wasiwasi.
“Nilipata hofu na kuongeza mwendo huku nikijitahidi kuzuia wasinipite, na kubadili mwelekeo na kuingia mtaa mwingine.
“Watu hao nao walikata kona na kunifuata, wakijaribu...