Baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza matokeo ya sensa, inayokaribia watu 45 milioni, siku chache baadaye deni la taifa lilitangazwa kufikia Sh21 trilioni huku katika wastani kila mtu akidaiwa Sh467,404. Fedha hizo zinatokana na mkopo baada ya Serikali kukopa kwa ajili ya kujenga miundombinu kama barabara, bomba la gesi, mishahara ya wafanyakazi, na miradi mingine. Kwa mujibu wa taasisi isiokuwa ya kiserikali ya Tanzania Coalition on Debt and Development (TCDD), serikali inadaiwa ‘mzigo wa madeni’ unaofika Sh21 trilioni.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo Hebroni Mwakagenda, anafafanua kwamba Serikali inakopa fedha hizo Benki Kuu (BoT), Benki za Biashara, Kampuni za Bima na Mashirika ya Hifadhi za Jamii, Benki ya Dunia (WB), Benki ya Maendeleo Afrika (ADB) na Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF).
Mwakagenda anasema deni limeongezeka kwa dola 456.1 milioni sawa na Sh7.3 trilioni katika kipindi cha mwaka mmoja tu, tangu Oktoba 2011.
Akichanganua kuhusu deni hilo Mwakagenda abainisha kuwa mpaka kufikia Oktoba mwaka jana, deni la nje lilikuwa Sh15.9 trilioni, kiwango ambacho ni cha juu kabisa kwa nchi kukopa kutoka ...