Pages

Nigerian Professor Claims to Have Found Possible Cure for HIV/AIDS

HIV/AIDS
A newspaper headline with the story in which a Nigerian prof. announced the development of a new drug that can cure HIV and AIDS.
He told the News Agency of Nigeria in Benin, that research on the project was started in 2010 and culminated in the development of “Deconcotion X (DX)–Liquid or Bioclean 11 for the cure of HIV and AIDS. He said the herbal drug had undergone “a series of successful tests.
Prof Ibeh told NAN,
We are at the threshold of making history, in the sense that we seem to have with us something that will permanently take care of what over time seems to have defied all solutions. We are talking about the latest discovery of an oral drug made from plants extraction in Nigeria for the possible cure for the pandemic, HIV and AIDS virus.
The existing retroviral drugs are intervention drugs for the management of AIDS but our new discovery is a possible cure. We have tried to look at the product first; its toxicological analysis and discovered that..

Mgao wa Umeme Haupo na Hautakuwepo, Bei Haitapanda,Tuvumilie Umeme uwe Unazimwa ili Tuboreshe Miundombinu - Prof. Muhongo!

 Prof. Muhongo
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amesema mwaka huu lazima alifumue Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kulisuka upya ili kukidhi mahitaji ya umeme.
Pia alisema Serikali, haitakubali kupandisha bei za umeme hadi hapo mapato na matumizi ya shirika hilo yatakapofanyiwa ukaguzi na kujiridhisha.
Profesa Muhongo, alitoa kauli hiyo mjini Dar es Salaam juzi, wakati akizungumza katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV mjini Dar es Salaam juzi.

Alisema msimamo wa Serikali, hadi sasa ni kwamba bei ya umeme haitapanda.
“EWURA na TANESCO, wamefuata taratibu zao za kubadilisha bei, lakini nimewaeleza na narudia kusisitiza chochote watakachojadili labda waje na bei ya kushusha umeme…Serikali haikubali bei ya kupandisha umeme huo ndio msimamo haubadiliki.
“Bei haitapanda, nimewaambia TANESCO kwamba endapo wanataka kupandisha bei ni lazima tukae chini na wao tuangalie matumizi yao ya fedha wanazozikusanya, sasa ikiwa kama matumizi yao ni makubwa hayaendani na hali halisi cha kwanza ni kufumua hilo shirika la TANESCO, nashukuru Watanzania walitoa maoni yao kuhusu muundo wa shirika wanalolitaka sasa yamekusanywa na wiki hii tutaletewa wizarani.
“Ujumbe wa mwaka wa 2013, ni lazima tufumue TANESCO tujenge upya ambayo itakidhi mahitaji yetu ya...

It's Mancini vs Balotelli

Mancini vs Balotelli
Mancini vs Balotelli
Mancini vs Balotelli
Mancini vs Balotelli

Kali TV Online: This Week's Around Town


In this first episode of 2013 Kali TV covers Black Girls Ignite Africa Workshop in Maryland which Chardelle Moore was invited to talk as Kali TV Host on her role as young woman in the media. Kali TV also travelled to NY to cover Yoliswa Cele US Africa Synergy Ambassador fundraising event which focuses on helping kids in Kwazulu Natal. We also featured Young African Professional Network (YAP) end of the year party and also visited Sibusiso Kunene a South African Immigrant who feeds homeless every tuesday in Washington DC.

Huenda Mwanamuziki Joseph Chameleone wa Uganda Akafunguliwa Mashitaka ya Mauaji!

Gazeti la Sunday Mail la Uganda limeripoti kwamba Polisi wa nchi hiyo wanaendesha uchunguzi ambapo huenda wakamfungulia mashitaka ya mauaji mwanamuziki Jose Chameleone, mke wake Daniella na kundi la muziki la Leon Island.
Ni kutokana na kifo cha Robert Karamagi (27) aliyefariki katika Hospitali ya Mulago baada ya majeraha aliyoyapata nyumbani kwa mwanamuziki huyo huko Seguku Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kajjansi Ibrahim Saiga alisema wamechukua ushahidi mbalimbali kutoka kwa majirani na mashuhuda walioona, ushahidi ambao unapingana na ule uliotolewa na familia ya Mayanja.
Pamoja na kusema faili la uchunguzi huo litapelekwa kwa Mwendesha Mashitaka wa Serikali (DPP) kwa ushauri, Saiga alisema pia baba wa Karamagi alikana kwamba mwanaye alijimwagia mafuta na kujiwasha moto, pia alisema mwanaye alipomwita hospitalini alimwambia aliteswa, akafungwa kamba, akamwagiwa mafuta na kuchomwa moto na mwanamuziki huyo pamoja na wenzake wa kundi lake.
Leon Island 
Jose Chameleone akihojiwa na NTV Uganda na kusema kwamba hilo swala wameliacha kwenye mikono ya polisi, gazeti la sunday mail limeripoti pia kwamba alhamisi iliyopita Jose Chameleone alihojiwa na wapelelezi kwa muda mrefu lakini aliachiwa kwa dhamana.

Jaji Mkuu Azindua Kitabu cha Sheria Chenye Maandiko ya Kesi Mbalimbali Pamoja na Jarida la Makala

Jaji Mkuu, Othuman Chande Jaji Mkuu, Othuman Chande akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha Sheria chenye maandiko ya kesi mbalimbali pamoja na jarida la makala, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), Jaji Engera Kileo na Msajili wa Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara.Picha na Prona Mumwi-Majira

Wanachuo Kipawa Sasa Kulipa Ada kwa M-Pesa

Chuo cha VETA kipawa
Wanachuo wa Chuo cha VETA Kipawa Dar es Salaam kuanzia sasa wataanza kulipa ada kupitia huduma ya M-Pesa baada ya chuo hicho kufikia makubaliano na Kampuni ya Simu za mikononi ya Vodacom kuwezesha huduma hiyo. Chuo hicho ni miongoni mwa Shule na Vyuo vingine kadhaa ambavyo vipo katika hatua za mwisho za mazungumzo na Vodacom ya kuviwezesha kutumia huduma ya M-pesa katika ulipaji wa karo ada nynegine katiika taasiis hizo za elimu nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo eneo la Kipawa kilipo chuo hicho Dar es Salaam, Mkuu wa Ukuzaji Biashara; M-Pesa Jackson Kiswaga amesema kuanza kwa huduma hiyo ni mwendelezo wa azima ya Vodacom ya kuyaleta maisha ya watanzania kiganjani kupitia teknolojia ya simu za mkononi. Amesema katika mipango ya kuwezesha malipo ya ..

Geto Boy Lyrics - Climax Bibo

Takin Over The Game - Wakazi

Wakazi

Mwandishi wa Redio Kwizera Issa Ngumba Ameuliwa Porini na Watu Wasiojulikana!!

Issa Ngumba.
Mwandishi wa habari wa Radio Kwizera anayefanyia kazi wilayani Kakonko mkoani Kigoma Bw. Issa Ngumba aliyepotea katika mazingita tata amekutwa amekufa na kunyofolewa sehemu zake za siri
Taarifa kutoka Kigoma zilizotufikia hivi punde zinadai kuwa mwili wa mwanahabari huyo umekutwa nje kidogo na mkoa wa Kigoma.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kigoma RPC Kishai amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa bado jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi .

Mbunge wa jimbo la Kigoma Zitto Kabwe pia amepata kuzungumza na mtandao huu na kudai kuwa ameguswa na kifo cha mtangazaji huyo na kutaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya kifo chake
Pia Kabwe ameeleza jinsi ambavyo mwanahabari huyo alivyoweza kuifanya kazi yake kwa jamii ya Kigoma kwa ufanisi zaidi na kuwa wakati mwingine yeye kama mbunge alikuwa akizunguka na mwanahabari huyo katika jimbo lake.
" Kweli nimeguswa sana na kifo cha kusikitisha cha mwanahabari huyo nilimfahamu vema kwa utendaji kazi wake ila nawapa pole sana waandishi wote nchini kwa msiba huu mkubwa .....na zaidi nitapata kueleza mengi mara baada ya uchunguzi"

Taarifa za awali zilizotolewa na Jeshi la Polisi wilayani Kakonko baada ya kupotea kwa mwanahabari huyo zilisema kuwa Bw Ngumba alipotea tangu January 05 mwaka huu majira ya saa 11 jioni ambapo alimuaga mke wake Bi. Rukia Yunus kuwa anakwendwa Muhange senta wilayani Kakonko na kwamba hajarudi nyumbani hadi sasa.
Kufuatia tukio hilo jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Muhange wanaendelea kumtafuta katika mapori ya kijiji hicho baada ya rafiki zake kueleza kuwa aliwaanga kuwa anakwenda kutafuta dawa msituni.
Issa Ngumba. 
Aidha jeshi la polisi Wilayani Kibondo liliomba kampuni za mitandao ya simu anayotumia Bw Ngumba kusaidia kutambua simu zake zilipotumika kwa mara ya mwisho ili kurahisisha upatikanaji wake. Akizungumza kwa njia ya simu, Mke wa Bw Issa Ngumba, Bi Rukia Yunus amesema kuwa wananchi walio wengi ambao walikuwa wakimtafuta maporini wamerudi kijiji hapo baada ya kumkosa.

Maswali yaliyo jitokeza!!
1. Kawaida redio hiyo hutangaza taarifa/habari za aina gani?
2. Ngumba amekuwa akiandika habari/taarifa za aina gani?
3. Je, ni mwandishi mwololo au ana mtima wa nyundo?
... 4. Je, ni mtafiti/mchunguzi na mchambuzi (alikuwa na kipindi maalum redioni)?
5. Mahusiano yake na wenzake yalikuwa ya namna gani?
6. Mahusiano yake na wenye chombo yalikuwaje?
7. Mara ya mwisho aliandika habari zipi (zilihusu nini, nani na wapi)?
8. Anafahamika kwa kuandika nini kilichosisimua nywele za wengi?
9. Kazi yake iliyowahi kuibua mjadala miongoni mwa wenzake, mwajiri na wasomaji?
10. Alikuwa anapanga kufanya nini/kufuatilia nini (kile ambacho wenzake walifahamu)?
11. Alikuwa na uhusiano wowote na polisi (upi)?
12. Uhusiano wake na watawala wilayani ulikuwa wa aina gani?
13. Je, ni mwandishi aliyejua mambo mengi na ya ndani ya utawala wilayani?
14. Je, ni mwandishi aliyejua biashara za wazi na siri za "wakubwa?"
15. Mbali na kituo chake cha redio, alikuwa akipeleka wapi kazi zake (zipi)?
16. Uhusiano na mkewe ulikuwa wa aina gani (kwa mujibu wa watu wa karibu)?
17. Alikuwa na tabia gani (majivuno, ukarimu, wepesi/uzito wa kuelewa, ushabiki wa mambo (yapi); au alikuwa mpigania haki, mpenda kujielimisha na mtafutaji aliyetaka kuleta mabadiliko katika kazi/maisha/familia yake (vipi)?
18. Alikuwa na watoto (wangapi, wako wapi)?
Maswali haya nimempelekea pia mwandishi Kayanda aliyeko Kigoma. Ni muhimu tujue angalau haya machache.