Pia alisema Serikali, haitakubali kupandisha bei za umeme hadi hapo mapato na matumizi ya shirika hilo yatakapofanyiwa ukaguzi na kujiridhisha.
Profesa Muhongo, alitoa kauli hiyo mjini Dar es Salaam juzi, wakati akizungumza katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV mjini Dar es Salaam juzi.
Alisema msimamo wa Serikali, hadi sasa ni kwamba bei ya umeme haitapanda.
“EWURA na TANESCO, wamefuata taratibu zao za kubadilisha bei, lakini nimewaeleza na narudia kusisitiza chochote watakachojadili labda waje na bei ya kushusha umeme…Serikali haikubali bei ya kupandisha umeme huo ndio msimamo haubadiliki.
“Bei haitapanda, nimewaambia TANESCO kwamba endapo wanataka kupandisha bei ni lazima tukae chini na wao tuangalie matumizi yao ya fedha wanazozikusanya, sasa ikiwa kama matumizi yao ni makubwa hayaendani na hali halisi cha kwanza ni kufumua hilo shirika la TANESCO, nashukuru Watanzania walitoa maoni yao kuhusu muundo wa shirika wanalolitaka sasa yamekusanywa na wiki hii tutaletewa wizarani.
“Ujumbe wa mwaka wa 2013, ni lazima tufumue TANESCO tujenge upya ambayo itakidhi mahitaji yetu ya...