
WALIMU wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Ruaruke wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, wameitelekeza shule hiyo kutokana na kukithiri kwa vitendo vya baadhi ya wanafunzi kuwadhalilisha kimapenzi, ikiwamo kuwabaka baadhi yao.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa mbali na udhalilishaji huo, wanafunzi hao wamekuwa wakiwatishia maisha walimu wao kwa namna mbalimbali. Katika moja ya vitisho hivyo, wamechoma moto nyumba zao tatu.
Habari hizo zimeeleza kwamba walimu hao wamelazimika kuikimbia shule hiyo baada ya baadhi ya walimu wa kike kutongozwa na wanafunzi, kupigwa mabusu kwa nguvu hadharani, kutishiwa kuchomwa visu na..