Pages

Kwa Watanzania Wanaoishi United Kingdom

Watanzania waishio UK mnaombwa kushirikiana kwa kuhudhuria hafla fupi ya kujitolea (harambee) kwa ajili ya kusaidia shughuli za usafirishaji na maziko ya watanzania wenzetu (Fredrick Mtoi na Mariagoreth Ndagio) vilivyotokea London na Luton.

Muda: Saa 11 jioni.
Siku: Alhamisi, 29 Nov.
Mahali: Tanzania High Comission UK
3 Stratford Place Marylebone
WC1 1AS. London

Ushirikiano wako ndiyo mafanikio ya shughuli hii muhimu. Kama hutaweza kuhudhuria tafadhali tuma mchango wako kwenye account ya Jumuiya:
TA (Tanzania Association)
HSBC
Sort Code: 40 05 26
A/C: 41 22 96 72

Jumla ya mchango utakaopatikana utagawanywa sawa kwa wahusika wa pande zote mbili. Iwapo ungependa mchango wako uelekezwe kwenye familia mojawapo tu, tafadhali bainisha kwa kuambatanisha ujumbe (simple note).
Asanteni kwa ushirikiano wenu

Tanzania National Associations (TANZ) UK

Sharo Milionea Kaiaga Dunia!!

DarSlam
Kuhusu kifo cha msanii/mwigizaji Sharo Milionea, namkariri Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo la Maguzonizonga wilayani Muheza hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza” Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei. Kwenye gari alikua mwenyewe.